Mechi ya Ngao ya
Jamii kati ya Azam Fc na Yanga Fc inayotarajiwa kuchezwa kesho katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam inatawanufaisha wanafunzi wa kwani sehemu ya mapato
itatumika kununulia madawati 200.
Akizungumza na
wandishi wa habari leo Afisa habari wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Alfred Lucas amesema kuwa mchezo huo
utaoneshwa na Ting kuptia chanel ya ATN
na sehemu ya mapato yapelekwa kwa katibu mkuu wa bunge, Dr. Kashilila kwani wao
wanaisaidia serikali kuchangia madawati.
“Ting wamepata haki
ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mechi ya kesho kama ambavyo huwa
wanarusha matangazo ya mechi ya ligi za Uingereza “ amesema Alfred
Naye Mkurugenzi
wa Michezo kutoka Ting, Dennis Msemo ameomba wadau kuhudhuria mchezo huo wa
ngao ya jamii
“Sisi
kupitia king’amuzi cha Ting tutaonesha mchezo kwenye chaneli ya ATN tunawaomba
wadau wote wa Michezo na Vyombo vya Habari kujumuika nasi pale uwanja wa Taifa
kuanzia saa kumi jioni, tunahitaji ushirikiano wetu wa hali na mali. Sisi
ajenda yetu kubwa ni michezo, na michezo kwetu ni utamaduni na hii ndio kauli
mbiu yetu” Amesema Dennis.
No comments:
Post a Comment