WANACHAMA wa klabu ya
Yanga Kanda ya Dar es Salaam wamempigia magoti na kumsihi abadili maamuzi yake
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, kubadili msimamo wake wa kutoikodi timu hiyo
Wanachama hao
wamemuomba Manji asibadili msimamo wake katika kikao cha dharura kilichoketi
leo kwenye makao Makuu ya timu hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Pia wanachama hao
wamekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa timu hiyo kuzungumza na vyombo vya
habari pasipo kupata ridhaa ya chama.
Mwenyekiti wa Matawi
ya Yanga Kanda ya Dar es Salaam, Robert Lyungu Kasera amemtaka katibu wa timu
hiyo Taifa kumfuta uanachama Katibu wa Baraza la wazee la Yanga Taifa, Ibrahim
Akilimali kwa madai kuwa kiongozi huyo anashirikiana na timu pinzani kukwamisha
mpango wa Manji kuikodi timu.
“Akilimali
anashirikiana na Simba kuiharibu Yanga hatufahi, haiwezekani aongelee masuala
ya Yanga pasipo ridhaa ya uongozi wa klabu mfikishe taarifa hii kwa usahihi
bila kumungunya na kikao hiki kinalaani kitendo alichofanya,” amesema Lyunga.
Zameda Mageka
mwanachama wa Yanga tawi la Wakali Temboni ameitaka Yanga kumsimamisha
Akilimali na kumteua Katibu mwengine kushika wadhifa wake.
Taarifa zisizo rasmi
zinadai kuwa uamuzi wa Manji kutaka kubwaga manyanga unatokana na kauli za
matusi na kejeli kutoka kwa baadhi ya viongozi wa ndani ya Yanga na serikalini.
No comments:
Post a Comment