WAJUMBE watatu wa Yanga ambao walivuliwa uanachama wamepeleka
barua yao kupinga hatua hiyo katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Akizungumza
na wandishi wa habari afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema barua hiyo iliwasilishwa
katika shirikisho hilo Agosti 12, 2016.
“Wanachama Ayoub Nyenzi, Hashim Abdallah na Mkemi ni
wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga ambao walivuliwa uanachama Agosti 6,
mwaka huu walileta barua ya malalamiko TFF, ” amesema Lucas.
Ameongeza kuwa
“nathibitisha kuwa malalamiko yao yamepokelewa ambayo yanalenga kutaka haki
itendeke.”
Amesema barua hiyo
inasema kuwa uongozi wa Yanga ulikiuka taratibu na katiba ya klabu hiyo
ilipowafuta uanachama.
“TFF imeyapokea
malalamiko hayo na yatapelekwa katika kamati husika pindi yatakapofanyiwa
maamuzi tutawajulisha wadau wa mpira wa miguu nchini,” amesema.
No comments:
Post a Comment