MSHAMBULIAJI
wa Simba, Laudit Mavugo amesema lazima
aongoze bidii ili kujihakikishia kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.
Akizungumza
na gazeti hili baada ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopard ya
Kenya, Mavugo kuanzia aanze mazoezi na
mchezo aliocheza amegundua upinzani ndani ya kikosi chao.
"Nimekuja
kucheza na ndiyo kazi yangu, lazima niongeze jitihada ili kuhalikisha napata
namba, sijaifahamu Simba kiundani ila kwa haraka haraka nimeona ni timu yenye
ushindani", alisema Mavugo
Kwenye
kikosi cha Simba kinachonolewa na Joseph Omog, Mavugo atakuwa na kazi ya
kuwania namba na Ame Ally, Ibrahim
Ajibu, Danny Lyanga na Fredric Blagnon ambaye ni raia wa Ivory Coast.
Mavugo
amesaini miaka miwili Simba akitokea Vital O ya Burundi na amesisitiza kuwa amekuja
Simba kulipa deni kwani mwaka jana alichukua
pesa ya usajili na hawakumshtaki kudai
haki yao baada kushindwa kutua Simba.
Katika
kusheherekea tamasha la Simba lililofanyika juzi, Mavugo alisherehesha furaha
ya wana Msimbazi baada ya kufunga bao la nne kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa
Taifa.
No comments:
Post a Comment