Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 9, 2016

JORDI MESTRE: NI AIBU NA KASHFA MESSI NA SUAREZ KUKOSA KWENYE LISTI YA TUZO MCHEZAJI BORA ULAYA


KUTOKUWEMO kwa Lionel Messi na Luis Suarez kwenye Listi ya Wagombea Watatu wa Tuzo ya UEFA ya MCHEZAJI BORA ULAYA 2015/16 kumedaiwa kuwa ni kashfa na Makamu wa Rais wa Barcelona Jordi Mestre.
Kukosena kwa Messi na Suarez, wote Wachezaji wa Barca, na kuwepo kwa Wachezaji Wawili wa Mahasimu wao Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale, na wa 3 kuwa Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, kumeifanya Barca ihuzunike na kukasirishwa sana kwa mujibu wa Mestre.
Hilo limewafanya Barca waone uchaguzi huo wa Watatu hao kugombea Tuzo hiyo kubwa Ulaya ambapo Mshindi atapatikana Agosti 25 iwe ni kashfa kubwa.
Ronaldo, Bale na Griezmann wametinga Fainali ya kugombea Tuzo hii kutoka Listi ya Wachezaji 10 baada ya kuzoa Kura za Wanahabari maalum kutoka Nchi 55 ambazo ndio Wanachama wa UEFA ambao pia ndio watakaopiga Kura hapo Agosti 25 huko Monaco wakati wa Droo ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI. 


Kwenye mchakato huo wa Wagombea 10 ili kupata Watatu wa Fainali, Messi, ambae amewahi kutwaa Ballon d'Or, Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani mara 5, alshika Nafasi ya 5 akiwa nyuma ya Suarez.
Lakini Mestre, akiongea na TV3, alisema: "Si sahihi. Sijui walitumia vigezo gani lakini sikubaliani nao. Kukosekana Wachezaji wetu Messi na Suarez ni kashfa. Klabu imehuzunishwa na kukasirishwa!"
Msimu uliopita wa 2015/6, Messi na Suarez waliibeba Barca kutwaa Ubingwa wa La Liga huku Messi akifunga Bao 41, 26 zikiwa za La Liga, wakati Suarez akichapa Bao 40 za La Liga na 59 kwa ujumla.
Mshindi wa Tuzo ya UEFA ya MCHEZAJI BORA kwa Mwaka Jana alikuwa Cristiano Ronaldo.