Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 13, 2016

RATIBA MECHI ZA MAN UNITED LIGI KUU ENGLAND YAREKEBISHWA KWA MWEZI OCTOBA NA NOVEMBA

MECHI 4 za Manchester United za Ligi Kuu England za Miezi ya Oktoba na Novemba zimebadilishwa kwa ajili ya kukidhi Matangazo Laivu ya TV ya huko Uingereza wakati zile Gemu dhidi ya Swansea City na West Ham United zimesogezwa na kuchomekwa Jumapili ili kuruhusu ushiriki wao kwenye UEFA EUROPA LIGI ambayo huchezwa Alhamisi Usiku.’
Man United wataanza kucheza UEFA EUROPA LIGI kwenye Makundi ambayo yatapangwa Agosti 26 na Mechi zake kuanza Septemba 15.
Mechi ya Man United na Stoke City itachezwa Jumapili Oktoba 2 na ule mtanange wa huko Anfield umesogezwa hadi Jumatatu Oktoba 17 na Wikiendi inayofuatia Jose Mourinho atatua Stamford Bridge kuivaa Klabu yake ya zamani Chelsea kwa mara ya kwanza.
Ile Mechi ya Old Trafford na Arsenal itachezwa Mchana hapo Jumamosi Novemba 19.

Man United – Ratiba Mechi zilizotenguliwa:
Manchester United v Stoke City, Jumapili Oktoba 2 Saa 1400
Liverpool v Manchester United, Jumatatu Oktoba 17 Saa 2200
Chelsea v Manchester United, Jumapili Oktoba 23 Saa 1800
Swansea City v Manchester United, Jumapili Novemba 6, Saa haijapangwa
Manchester United v Arsenal, Jumamosi Novemba 19, Saa 1530
Manchester United v West Ham United, Jumapili Novemba 27 saa 1930