Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 27, 2016

CRISTIANO RONALDO MCHEZAJI BORA ULAYA


MCHEZAJI wa Real Madrid na Kepteni wa Timu ya Taifa ya Portugal, Cristiano Ronaldo, ametwaa Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa Msimu wa 2015/16.
Ronaldo aliwabwaga Gareth Bale, ambae wanacheza wote Real Madrid, na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid kwenye Kura ambazo zimepigwa na Wanahabari maalum kutoka Nchi zote 55 Wanachama wa UEFA.
Hii ni mara ya Pili kwa Ronaldo kutwaa Tuzo hii.

Ronaldo alikuwa na Msimu mzuri wa 2015/16 akivuka Bao 50 kwa mara ya 6 mfululizo, yaani Miaka 6, katika Msimu mmoja akiichezea Real Madrid.
Kwenye UCL, Ronaldo aliibuka Mfungaji Bora akifikia Rekodi ya Bao 16 na Penati yake ndio iliipa ushindi Real kuibwaga Atletico katika Fainali kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano na kutwaa Ubingwa huko Milan.
Akiwa na Portgugal huko EURO 2016, Ronaldo alifunga Bao 3 na kutoa msaada mara 2 wakitwaa Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza katika Historia yao.
Washindi waliopita wa Tuzo hii ni Lionel Messi (2011, 2015), Andrés Iniesta (2012), Franck Ribéry (2013) na Ronaldo (2014).


ZIFUATAZO NI SIFA ZA KILA MGOMBEA KWA MSIMU WA 2015/16:

Gareth Bale
Bale alisaidia sana Klabu yake Real Madrid hadi kutwaa Ubingwa wa UCL.
Kwenye Fainali ya UCL, yeye ndie alietoa msaada kwa Sergio Ramos kufunga Bao la kwanza dhidi ya Atletico Madrid na pia kufunga Bao kwa Penati katika Mikwaju ya Penati Tano Tano.
Kwenye EURO 2016 Mwaka huu huko France, Bale alifunga Bao 3 kuisaidia Nchi yake Wales kufanya vizuri.
Hakuwemo kwenye Timu Bora ya EURO 2016.

Antoine Griezmann
Griezmann aliichezea vizuri Atletico Madrid, akiwa Mfungaji Bora wao kwa kufunga Bao 22 kwenye La Liga na kumaliza Pointi 3 nyuma ya Mabingwa Barcelona.
Kwenye UCL, ambako walibwagwa na Real Madrid, Griezmann alifunga Bao 7 katika Gemu 13.
Akiwa na France kwenye EURO 2016, Griezmann ambako alifunga Bao 6 na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano hayo alipoisaidia France kufika Fainali na kubwagwa na Portugal.

Cristiano Ronaldo
Ronaldo alikuwa na Msimu mzuri wa 2015/16 akivuka Bao 50 kwa mara ya 6 mfululizo katika Msimu mmoja akiichezea Real Madrid.
Kwenye UCL, Ronaldo aliibuka Mfungaji Bora akifikia Rekodi ya Bao 16 na Penati yake ndio iliipa ushindi kuibwaga Atletico katika Fainali kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano na kutwaa Ubingwa huko Milan.
Akiwa na Portgugal huko EURO 2016, Ronaldo alifunga Bao 3 na kutoa msaada mara 2 wakitwaa Ubingwa wa Ulaya.
Akiwa ametwaa Makombe Mawili makubwa na Magoli kibao ni ngumu kumfuta Ronaldo kutwaa Tuzo hii.

No comments:

Post a Comment