Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 4, 2016

TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUANZA WIKI IJAYOTIKETI za elektroniki zitaanza kutumika wiki ijayo katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya miundombinu kukamilika.
Kauli hiyo ilisemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. wakati akipokea mkanda WBF kutoka kwa bondia Francis Cheka.
Tumekubaliana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa tiketi za elektroniki zianze kutumika baada ya michezo ya Machi 8,  ili TFF wamalize tiketi walizokuwa wamechapisha, alisema Nape.
Pia Nape alisema miundombinu ya kuruhusu matumizi ya hizo tiketi yamekamilika kama Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alivyoagiza alipokutana na wadau na viongozi wa vyama vya michezo hivi karibuni.
Nape pia alimpongeza bondia Cheka kwa kumpiga bondia  wa Serbia, Geard Ajetovic katika pambano la kuwania ubingwa WBF ambalo lilifanyika viwanja vya Leaders Klabu, Dar es Salaam hivi karibuni.
Kwa niaba ya Watanzania nakupongeza kwa kumpiga Ajetovic ndani ya ardhi ya nchi yako na sisi Wizara inayosimamia michezo tutajitahidi kuwasaidia wanamichezo wote kufanikisha malengo yao, alisema Nape.
Naye Cheka alitoa shukrani zake kwa Watanzania ambao walijitokeza kumuunga mkono katika pambano hilo na kuomba kampuni zijitokeze kuwekeza katika michezo.