Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 27, 2016

EUROPA LEAGUE, MAKUNDI: MAN UNITED YAPANGWA NA FENERBAHCE, FEYENOORD, ZORYA, GENK YA SAMATTA NA BILBAO, VIENNA NA SASSUOLO

 
DROO ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI imefanyika hii Leo huko Monaco na Makundi 12 ya Timu 4 kila moja yamepatikana.
Mechi za kwanza za Makundi zitachezwa Septemba 15.

DROO KAMILI:
KUNDI A: Manchester United, Fenerbahce, Feyenoord, Zorya
KUNDI B: Olympiacos, Apoel, Young Boys, FC Astana
KUNDI C: Anderlecht, St Etienne, Mainz, Qabala
KUNDI D: Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar, Maccabi Haifa, Dundalk
KUNDI E: Viktoria Pizen, AS Roma, Vienna, Astra Giurgiu
KUNDI F: Athletic Bilbao,KRC Genk, Rapid Vienna, Sassuolo
KUNDI G: Ajax, Standard Liege, Celta Vigo, Panathinaikos
KUNDI H: Shakhtar Donetsk, Braga, Gent, Konyaspor
KUNDI I: Schalke, Salzburg, Krasnodar, Nice
KUNDI J: Fiorentina, PAOK, Slovan Liberec, Qarabag
KUNDI K: Inter Milan, Spata Praga, Southampton, Hapoel Be’er Sheva
KUNDI L: Athletic Bilbao, Steau Bucharest, FC Zurich, 


Manchester United watakutana na klabu anayochezea nyota wao wa zamani Robin Van Persie- Fenerbahce- pamoja na Feyenoord na Zorya Luhansk hatua ya makundi Europa League.
Klabu ya KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Ally Samatta imewekwa kundi F na Athletic Bilbao ya Uhispania, Rapid Vienna ya Austria na Unione Sportiva Sassuolo Calcio kwa ufupi Sassuolo ya Italia.
Southampton, klabu nyingine ya Ligi ya England inayocheza michuano hiyo, imepangwa kucheza dhidi ya Inter Milan, Sparta Prague na Hapoel Beer Sheva.

Dundalk ya Ireland nayo imepangwa na h Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar na Maccabi Tel-Aviv baada ya droo kufanywa Monaco.

Meneja wa United Jose Mourinho amesema hawafahamu vyema wapinzani wao Zorya, kutoka Ukraine, lakini amefurahia kuwekwa kundi moja na Fenerbahce na Feyenoord.

"Sote twafahamu kwamba shindano hili si kama Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya lakini kuwa na Manchester United ikikutana na klabu zenye historia ndefu kama vile Fenerbahce na Feyenoord ni jambo zuri kwetu," amesema.


TAREHE MUHIMU
Droo

26/08/16: Makundi
12/12/16: Raundi ya Mtoano ya Timu 32
24/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16
17/03/17: Robo Fainali

Makundi
15/09/16: Mechidei 1
29/09/16: Mechidei 2
20/10/16: Mechidei 3
03/11/16: Mechidei 4
24/11/16: Mechidei 5
08/12/16: Mechidei 6

16/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi za Kwanza
23/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Marudiano
09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza
16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano
13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza
20/04/17: Robo Fainali, Marudiano
04/05/17: Nusu Fainali, Mechi za Kwanza
11/05/17: Nusu Fainali, Marudiano
24/05/17: Fainali (Friends Arena, Solna, Stockholm, Sweden)