|
Kajala akiwa na Wema Sepetu mara baada ya kuachiwa huru baada ya Wema kumlipia milioni 13 |
MSANII maarufu nchini, Wema Sepetu amemnusuru msanii mwenzake Kajala Masanja kwenda jela miaka saba baada ya kumlipia faini ya fedha taslimu ya Sh.milioni 13 .
Hata hivyo wakati Kajala
akiachiwa huru, mumewe Faraja Chambo amehukumiwa kifungo cha miaka 12
jela kutokana na kushindwa kulipa faini ya Sh milioni 213.
Mke na mume hao
walihukumiwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi
Sundi Fimbo baada ya kuwatia hatiani kwa makosa matatu ya kula njama, kuuza
nyumba iliyopatikana katika mazingira ya rushwa ili kuficha ukweli na kosa la
utakatishaji fedha.
Mahakama ya Kisutu
ilitawaliwa na vituko mbalimbali kwani wakati hukumu ikisomwa, Kajala alikuwa
akilia muda wote hali iliyosababisha wasanii wengi waliojaa mahakamani kuangua
vilio kwa kububujikwa na machozi kwani hawakuweza kutoa sauti wakihofia
kukamatwa kwa kuisumbua mahakama.Hakimu Fimbo alipomaliza kusoma hukumu Kajala
alijikuta akikaa chini na kulia kwa huzuni, alitolewa nje kuelekea mahabusu na
kuwaacha wasanii wakilia na kupanga jinsi ya kumsaidia aweze kutoka
gerezani.
Mama mzazi wa Faraja
alitoka mahakamani na kuelekea katika mahakama nyingine ya wazi, alipofika humo
aliangua kilio kikubwa kilichovuta watu kumfata kujua kulikoni, mama huyo
alivua viatu na kuanza kuwakimbiza wapiga picha walioanza kumpiga picha.
Kuwakimbiza na
kuwarushia mkoba wake hakuona kama inatosha aliamua kuokota mawe na kuwatishia
kuwapiga nayo, walifanikiwa kumpiga picha lakini walikuja kuondolewa na askari
kwa ajili ya utulivu.
Wasanii walianza
kuchanga fedha kwa ajili ya kulipa faini ya jumla ya Sh milioni 13 lakini Wema
aliwakataza na kuwaambia kwamba fedha zote atazilipa, aliondoka eneo hilo
kuelekea benki na baada ya masaa mawili alirudi na fedha hizo.
Akisoma hukumu, Hakimu
Fimbo alisema upande wa amshtaka katika kesi hiyo ulikuwa na mashahidi saba na
waliweza kuthibitisha katika ushahidi wao kwamba washtakiwa walitenda
makosa hayo huku wakijua.
"Kuna makosa matatu,
kosa la kwanza wanadaiwa Aprili, 2010 walikula njama ya kuuza nyumba iliyokuwa
Kunduchi Sala sala jijini Dar es Salaam, Shtaka la pili kuuza nyumba hiyo
Aprili 14, 2010 kwa Emiliana Rwegangira huku wakijua kuna notisi
inayowakata kufanya hivyo na shtaka la tatu la kutakatisha fedha.
"Ili mahakama itoe
uamuzi kwa kosa la kula njama lazima iangalie kosa la pili la kuuza nyumba
iliyozuiliwa kuuzwa kwa sababu ilipatikana katika kwa nia ya rushwa, kwa
kuangalia ushahidi mahakama inawatia hatiani kwa kosa la pili,"alisema
Fimbo.
Alisema kwa kuwa shtaka
la pili wametiwa hatiani, mahakama inawatia hatiani kwa shtaka la kulanjama
kwani limethibitika. Katika shataka la tatu la kutakatisha fedha, mahakama
inamtia hatiani mshtakiwa Faraja na kumwachia huru Faraja kwa sababu alihusika
katika kuuza nyumba lakini hajui fedha za kujenga nyumba hiyo zilipatikanaje.
"Kwa kosa la kwanza
la kula njama, mahakama inawatia hatiani washtakiwa wote na watalipa faini ya
Sh milioni 5 au kwenda jela miaka miwili kama watashindwa kulipa, Shtaka la
pili washtakiwa wote watakwenda jela miaka mitano kama watashindwa kulipa faini
ya Sh milioni 8 na shtaka la tatu faraja anatakiwa kwenda jela miaka
mitano akishindwa kulipa faini ya Sh milioni 200,"alisema.
Baada ya kutoa adhabu
hizo wasanii walihaha kuchangishana lakini Wema aliokoa jahazi kwa kutoa jumla
ya Sh milioni 13 kwa ajili ya kumuokoa Kajala ambaye baada ya saa tatu
alifanikiwa kutoa kuelekea nyumbani.Kajala aliondoka na gari la kifahari eneo
la Mahakama ya Kisutu kwa kulakiwa na ndugu, jamaa na marafiki waliokuwepo eneo
hilo.
Kajala na mumewe
walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, Machi 15, mwaka jana na
kusomewa mashitaka matatu ya kula njama, kubadilisha umiliki wa nyumba
baada ya kuiuza na kutakatisha fedha haramu, kosa ambalo halina dhamana
kisheria.
Washitakiwa hao
wanadaiwa kula njama ya kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi, Salasala,
Dar es Salaam, kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Pia, wanadaiwa Aprili 14,
2010, walihamisha umiliki wa nyumba kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa.Kajala na mumewe wanadaiwa katika shitaka la tatu kuwa, April 14,
2010, wakijua kuwa ni kinyume na sheria, walifanya kosa la kutakatisha
fedha haramu.
Kajala na mumewe
wanadaiwa katika shitaka la tatu kuwa, Aprili 14, 2010, wakijua kuwa
ni kinyume na sheria, walifanya kosa la kutakatisha fedha haramu.
"Hakuna ubishi kwamba washtakiwa walikaa wakaamua kuuza
nyumba, kinachotakiwa kuangalia kama kweli walifanya hivyo kihalali au la kwani
ushahidi ulionyesha washtakiwa wote walishiriki katika utaratibu wa kuuza
nyumba hiyo.
Namshauri Wema abadirike kwani hizo pesa atakuja kuzijutia kwa kuuza sura kwenye magazeti.Atembelee mahospitalini ,Shule za vijijini,ajionee jinsi watu wanavyoishi katika mazingira magumu kuna wagonjwa wa kansa ambao wanahitaji msaada wao.
ReplyDeleteSijafurahishwa kabisa kwa kitendo cha wema kujinadi kwenye vyombo vya habari na kuuza sura namshauri abadirike kwani kuna watu wana matatizo zaidi ya hayo,Wagonjwa,Mayatima,Pia angetembelea vijijini na kujionea jinsi wanafunzi wanavyokaa chini kwa ukosefu wa madawati kuriko kuwasaidia watu ambao walifanya kosa kwa faida zao.
ReplyDeleteDada wema hii ni tawab kwa mungu na kwa hakika mungu azidi kuku jazia baraka .ila tembelea hata vyou vya mayatima nao uwasaidie na kwa hakika watoto hao hawatakusahau katika maombi .
ReplyDelete