Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, June 21, 2016

TFF YAOMBA UZALENDO KWENYE MCHEZO WA YANGA NA TP MAZEMBE NA ULE WA SERENGETI BOYS



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF)  limewataka mashabiki kuwa wazalendo kwa kushangilia kistaarabu timu ya Taifa ya Vijana 'Serengeti Boys na ule wa Yanga kwani zinawakilisha taifa letu.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred Lucas, TFF inawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kushangilia kwani wanaamini mashabiki ni mchezaji wa 12 na uwepo wao utaongeza ari ya ushindi.
"Tunafahamu mchezo wa Yanga utakuwa na changamoto zake kwa vile  wameanza kwa kufungwa na TP Mazembe wanaongoza kundi lakini tunaamini watafanya vizuri kwani inachezwa kwa mtindo wa ligi hivyo mashabiki waje kushangilia timu zetu.", alisema Lucas.
Yanga itacheza na TP Mazembe Juni 28 kwenye mchezo wa Kundi A wa kombe la shirikisho barani Afrika na Serengeti Boys itacheza na Shelisheli mchezo wa kuwania kufuzu fainali za vijana barani Afrika, Jumapili
Mchezo wa Yanga utachezwa na mwamuzi wa kimataifa toka Zambia, Janny Sikazwe na atasaidiwa na Jerson Emiliano toka Angola na Berhe O'Michael toka Eritrea wakati mezani atakuwepo Wellington Kaoma toka Zambia.
Kamishna wa mchezo huo ni Celestin Mtagungira toka Rwanda wakati mratibu wa mchezzo huo ni  Sidio Mugadza toka Msumbuji.
Kwa upande wa Serebgeti Boys, mchezo huo utachezeshwa na waamuzi toka Ethiopia ambao ni Belay Asserese akisaidiwa na Tigle Bilachew na Kinfe Yilma na mezani atakuwepo Lemma Nigussie na kamishina atakuwa Kalombo Bester toka Malawi.
Yanga inatarajia kurejea nchini wakati wowote ikitoka Algeria ambapo ilikwenda kucheza na Mo Bejaia ambapo ilifungwa bao 1-0.

No comments:

Post a Comment