Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, June 18, 2016

YANGA YANASA MKALI MWINGINE TOKA ZIMBABWE

Obrey Chirwa alivyowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Dar es SalaamObrey Chirwa (katikati) akisaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Yanga, kushoto ni Mjumbe wa kamati ya mashindano ya Yanga Mustapha Urungu na kulia ni Wakili Jacqueline Majule aliyesimamia zoezi hilo


Mshambuliaji raia wa Zambia, Obrey Chirwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Yanga.
Chirwa ambaye alikuwa anaichezea FC Platinum ya Zimbabwe, amewasili jana Dar es Salaam na kukamilisha taratibu za usajili.
Yanga imekamilisha idadi ya wachezaji saba wa kimataifa kwa mujibu wa kanuni na sheria za TFF na nyongeza ya wachezaji watano kwa mijibu wa usajili wa CAF.
Nyota huyo anaungana na wachezaji wengine waliowahi kuichezea FC Platinum Donald Ngoma na Thaban Kamusoko ambao walisajiliwa msimu uliopita.
Klabu ya FC Platinum imethibitisha pia nyota huyo kujiunga na Yanga kwa kuandika ujumbe kwenye akaunti rasmi ya klabu hiyo uliosomeka: “Obreu Chirwa amejiunga rasmi na klabu ya Young Africans ya Tanzania kwa mkataba wa muda mrefu na kumtakia kila laheri kwenye safari yako mpya,” 
Kwa hisani ya Shaffih blog

No comments:

Post a Comment