Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, June 21, 2016

JOSE MOURINHO KUMNASA NEMANJA MATIC WA CHELSEA


MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho anatarajiwa kumchukua Mchezaji wa Chelsea kwa kubadilishana na Mchezaji wake mmoja kwa mujibu wa ripoti toka huko England.
Huku Dirisha la Uhamisho likikaribia kufunguliwa rasmi hapo Julai Mosi, imeripotiwa kuwa Mourinho anatarajiwa kuitumia shauku ya Meneja mpya wa Chelsea kutoka Italy, Antonio Conte, ya kumhusudu Beki toka Italy, Matteo Darmian, kwa kumtoa kama Ofa ya kumchukua Kiungo wa Chelsea Nemanja Matic.

Tayari Mourinho ameshaanza kuisuka upya Man United kwa kumnunua Sentahafu kutoka Villareal Eric Bailly na anatarajiwa kuongeza wapya wengine.

Matic, Mchezaji wa Kimataifa wa Serbia, ndie alikuwa Mchezaji wa kwanza Mourinho kumnunua aliporudi Chelsea kwa mara ya pili kwa kumsaini Mwaka 2014 kutoka Benfica na sasa inaelekea Mourinho anataka kuungana tena na Matic.

Chini ya Mourinho, Matic alipata Msimu mzuri wa kwanza huko Stamford Bridge na kuweza kutwaa Ubingwa wa England lakini Msimu uliopita, na hasa Mourinho alipotimuliwa Mwezi Desemba, Matic amekuwa hana namba mara kwa mara.

Hadi sasa haijulikani kama Matic atakuwa vipi chini ya Meneja mpya Conte ambae bado hajatua rasmi huko Chelsea kwani yupo bado kama Kocha wa Timu ya Taifa ya Italy ambayo sasa ipo France kwa ajili ya Fainali za EURO 2016.

Magazeti huko England yamedai Darmian yupo kwenye uhusiano mzuri na Conte kwenye Timu ya Italy kwani panga pangua hakosi namba na hilo limeleta Imani kuwa anamtaka wawe wote huko Chelsea.

Darmian amekuwa na Msimu mchanganyiko huko Man United ambako alitua Mwaka Jana kutoka Klabu ya Italy Torino na hilo, pengine, ndio linamfanya Mourinho amtoe kafara ili amnase Kiungo Matic ambae hucheza kwa miguvu katikati ili kuimarisha safu hiyo ambayo ni dhaifu kwa Timu hiyo.

No comments:

Post a Comment