Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 27, 2016

JOSE MOURINHO ASISITIZA KUSAHAU YALIYOPITA

José Mourinho ndie Meneja mpya wa Manchester United kwa Msimu wa 2016/17 baada ya kusaini Mkataba wa Miaka Mitatu ambao pia unaweza kumuweka hadi Mwaka 2020.
José, Raia wa Ureno mwenye Miaka 53 na ambae ametwaa Makombe 22 tangu 2003, amefundisha Klabu kadhaa kubwaa Ulaya na kutwaa Mtaji katika Nchi 4 tofauti (Portugal, England, Italy na Spain) ikiwa pamoja na kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI, mara 2 akiwa na FC Porto 2004 na Inter Milan 2010.

Akitangaza rasmi uteuzi huu, Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United Ed Woodward, alisema: “Jose ni Meneja Bora kabisa kwenye Gemu hivi sasa. Ametwaa Mataji na kuhamasisha Wachezaji katika Nchi kadhaa Ulaya na pia anaijua Ligi Kuu England nje ndani ambako ametwaa Ubingwa mara 3! Namkaribisha Manchester United!”

Nae José Mourinho amesema: "Kuwa Meneja wa Manchester United ni heshima spesho katika Gemu. Ni Klabu inayojulikana na inayopendwa Dunia nzima. Kuna kitu cha ajabu na mapenzi ambacho Klabu nyingine yeyote hawana!”
Aliongeza: “Siku zote nimekuwa na mvuto mkubwa na Old Trafford, na huu umekuwa ni Uwanja wenye kumbukumbu muhimu kwangu na pia Mashabiki wao tuko vyema. Sasa nina hamu kubwa kuwa Meneja wao na kufurahia sapoti yao kwa Miaka ijayo!”Zlatan Ibrahimovic kutua nae Old Trafford

No comments:

Post a Comment