Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 17, 2016

DHARAU ZAMPONZA BEKI WA LIVERPOOL, ATEMWA CROATIA YA EURO 2016

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Croatia Ante Cacic ameacha kumchukua Beki wa Liverpool Dejan Lovren kwenye Kikosi chake cha kushiriki Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, zitakazochezwa huko France kuanzia Juni 10 kwa kile alichodai ni kuwa na dharau.
Kocha Ante Cacic ameteua Wachezaji 27 ambao watabikishwa 23 kabla ya EURO 2016 kuanza.
Kuachwa kwa Lovren kunatokana na Beki huyo kutochezeshwa kwenye Mechi waliyotoka Sare 1-1 na Hungary na yeye kuwa Benchi na kisha kuambiwa apashe moto lakini hakuingizwa kucheza.
Alipogundua kuwa hataingizwa kucheza Mechi hiyo, Lovren akakasirika na kuacha kupasha moto na baadae kutoa maneno ya hasira kwa Kocha Cacic.
Kocha huyo ameeleza kuwa kuichezea Timu ya Taifa kunahitaji uwe mzuri na utumikie vizuri Klabu na Timu ya Taifa.
Cacic ameeleza: “Sijamfungia mlango Lovren. Iko Siku atarudi akigundua kuwa Mchezo huu ni wa Kitimu. Akishajua kutodharau Wachezaji wenzake, Wafanyakazi na Kocha atapata njia ya kurudi.”
Kwenye EURO 2016, Croatia ipo Kundi D pamoja na Mabingwa Watetezi Spain, Czech Republic na Turkey.

CROATIA -Kikosi kamili cha Wachezaji 27:

MAKIPA: Danijel Subasic (Monaco), Lovre Kalinic (Hajduk Split), Ivan Vargic (Rijeka), Dominik Livakovic (Dinamo Zagreb)

MABEKI: Vedran Corluka (Lokomotiv Moscow), Darijo Srna (Shakhtar Donetsk), Domagoj Vida (Dynamo Kiev), Sime Vrsaljko (Sassuolo), Gordon Schildenfeld (Dinamo Zagreb), Ivan Strinic (Napoli), Tin Jedvaj (Bayer Leverkusen), Duje Caleta-Car (Red Bull Salzburg)

VIUNGO:
Luka Modric (Real Madrid), Ivan Rakitic (Barcelona), Mateo Kovacic (Real Madrid), Marcelo Brozovic (Inter Milan), Milan Badelj (Fiorentina), Ivan Perisic (Inter Milan), Alen Halilovic (Sporting Gijon), Domagoj Antolic (Dinamo Zagreb), Marko Rog (Dinamo Zagreb), Ante Coric (Dinamo Zagreb)

MASTRAIKA: Mario Mandzukic (Juventus), Nikola Kalinic (Fiorentina), Marko Pjaca (Dinamo Zagreb), Andrej Kramaric (Leicester City), Duje Cop (Dinamo Zagreb)

No comments:

Post a Comment