Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 17, 2016

CHELSEA, SPUR WAPIGWA FAINI NA FA NA ONYO KALI JUU

FA, Chama cha Soka England, kimeshusha Faini kubwa kwa Klabu za Chelsea na Tottenham kwa makosa ya kushindwa kudhibiti Wachezaji wao wakati Timu hizo zilipopambana kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Stamford Bridge na kutoka Sare ya 2-2 ambayo iliwapa Ubingwa Leicester City hapo Mei 2.
Chelsea wametwangwa Faini ya Pauni 375,000 na Spurs kupigwa Faini ya Pauni 225,000 baada ya Klabu zote mbili kukiri makossa yao matatu ya kushindwa kudhibiti Wachezaji na Maafisa wao.
Kwenye Mechi hiyo Wachezaji 9 wa Spurs walipewa Kadi za Njano huku Kiungo wao Mousa Dembele baadae akifungiwa Mechi 6 kwa kumtia kidole Machoni Straika wa Chelsea Diego Costa katika moja ya rabsha kadhaa za Wachezaji katika Mechi hiyo.

Wachezaji Watatu wa Chelsea nao walipewa Kadi za Njano katika Mechi ambayo mwishoni baada ya kumalizika lilitokea zogo kubwa kati ya Wachezaji wa Chelsea na Spurs pamoja na Maafisa wa pande hizo mbili kuingilia na kusababisha Meneja wa muda wa Chelsea Guus Hiddink ale mweleka hadi chini.

Ikitangaza hukumu hizo, FA imesema Klabu hizo zimekiri Makosa Matatu ya kuvunja Sheria ya FA E20 kwa kushindwa kudhibiti Wachezaji na Maafisa wao katika Matukio yaliyotokea Dakika za 45 na 87 za Mechi hiyo na pia mwishoni mwa Mechi hiyo.

Pia, FA imesema Klabu hizo zimekung’utwa Faini kubwa kwa sababu Chelsea imeshawahi kupatikana na hatia ya kuvunja Sheria hiyo hiyo mara 4 Msimu huu na Spurs mara 2 tangu Novemba 2014.
Klabu zote mbili zimepewa Onyo kali na kutakiwa kuchunga mwenendo wao wa baadae