Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 17, 2016

CLAUDIO RANIERI MENEJA BORA ENGLAND

Claudio Ranieri after receiving the LMA Manager of the Year 2016 awardClaudio Ranieri akiwa na Tuzo yake mkononi BOSI wa Mabingwa wapya wa England Leicester, Claudio Ranieri, ametwaa Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka wa England.
Ranieri, Raia wa Italy mwenye Miaka 64, amezoa Tuzo hiyo iliyotolewa na LMA, League Managers' Association, Chama cha Mamenej wa Ligi huko England, kwa kuiongoza Leicester kutwaa Ubingwa wao wa kwanza katika Histiria ya Klabu yao ya Miaka 132.
Mbali ya Tuzo hiyo, Pia Ranieri alipewa Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka kwa Ligi Kuu England ambapo MTuzo nyingine zilikwenda za Mameneja wa Madaraja tofauti zilikwenda kwa Chris Hughton wa Brighton alitwaa ile ya Daraja la Championship, Gary Caldwell wa Wigan alitwaa ya Ligi 1 na Chris Wilder wa Northampton kutwaa ya Ligi 2.

Ranieri amekuwa Mtu wa Pili baada ya Arsene Wenger, alietwaa Mwaka 2002 na 2004, kuzoa Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka wakati si Mwingereza au kutoka Ireland.
Msimu huu, Ranieri alizoa Tuzo za Meneja Bora wa Ligi Kuu England mara 3 na huko kwao Italy pia ametunukiwa kuwa ndie Meneja Bora wa Mwaka.

Pia, Chris Hughton amekuwa Mtu wa Kwanza kutwaa Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka wakati Timu yake Brighton haikutwaa Ubingwa wa Daraja lake ambapo kikawaida yule Meneja anaeiongoza Timu yake kutwaa Ubingwa wa Daraja lake ndie hutunukiwa Tuzo hii.

Brighton walimaliza Nafasi ya Tatu kwenye Ligi ya Daraja la Pili, Championship, na Jana walitupwa nje ya Mchujo wa kusaka Timu ya Tatu kuungana na Burnley na Middlesbrough kupanda Daraja kuingia Ligi Kuu England baada ya kutolewa na Sheffield Wednesday

No comments:

Post a Comment