Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 19, 2016

MKWASA AMREJESHA VANAVARO LICHA YA KUTANGAZA KUJIUZULU
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Boniface Mkwasa amemrejesha kwenye kikosi nahodha wa zamani Nadir Haroub Canavaro kuziba nafasi ya Kelvin Yondani ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano hivyo kuikosa mechi ya Misri Juni 4.
Mkwasa  alitaja kikosi chenye majina ya wachezaji 27 kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya pamoja na ile ya kufuzu kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri na kujumuisha jina la nahodha wa zamani aliyejiuzulu Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Kikosi cha Taifa Stars kitaingia kambini tarehe 23 kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya utakaochezwa tarehe 29 Mei jijini Nairobi.
Baada ya hapo Taifa Stars itarejea Dar kukamilisha maandalizi ya kuivaa Misri katika mchezo ambao inahitaji ushindi wa angalau mabao matatu kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon mwakani.


Kikosi kamili cha Stars: 
Walinda Milango: Deo Munish (Yanga), Aishi Manula (Azam) Benno Kakolanya (Prisons).
Walinzi: Juma Abdul, Haji Mwinyi, Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris (Azam), Mohamed Tshabalala (Simba), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar).
Viungo: Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar),Hassan Kabunda (Mwadui), Juma Mahadhi (Coastal Union), Ismail Issa Juma (JKU).
Washambuliaji: Elias Maguri (Stand United), John Bocco (Azam) Ibrahim Hajib (Simba), Mbwana Samatta (Genk GRC, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe)