Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 19, 2016

ROY KEANE: MAN UNITED WANACHEZA KAMA HAWAJUANI KABISA


KEPTENI wa zamani wa Manchester United Roy Keane amesikitishwa na jinsi timu yake hiyo ya zamani ilivyotupwa nje ya UEFA EUROPA LIGI huku akionya Wachezaji hao chini ya Louis van Gaal hawana moyo wa ujasiri.
Jana Man United walitoka sare 1-1 na Liverpool Uwanjani Old Trafford na kutupwa nje ya EUROPA LIGI kwa vile walifungwa 2-0 katika Mechi ya kwanza huko Anfield Wiki iliyopita.
Man United hivi sasa wapo Nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu England na wanapaswa kurudiana na West Ham huko Upton Park ikiwa watataka kutinga Robo Fainali ya FA CUP baada kutoka 1-1 huko Old Trafford.
Akiongea kwenye Kituo cha ITV ya Uingereza, Keane alisema: "Nimehuzunishwa sana kuiona Man United ilivyo katika Mwaka mmoja na miwili iliyopita. Ni kama vile kundi la wageni limekusanywa na kutupwa Timu moja kucheza. Ukiichezea United na kuivaa ile Jezi unapaswa kuwa na moyo wa ujasiri. Siku zote nilikuwa najiona nina urefu wa Futi 10!"
Aliongeza: "Ukiwaona hawa Wachezaji wa sasa ni wazi wana presha wanaonyesha mchecheto kuivaa Jezi ya United. Najua wana majeruhi. Hali hii inaonyesha umuhimu wa Wayne Rooney.Nikitazama hawa wengine, hamna shujaa, kiongozi!"