Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 18, 2016

TWIGA KUONDOKA LEO USIKU KWENDA ZIMBABWE




TIMU ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu “Twiga Stars” imeondoka jana usiku kwenda nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake utakaochezwa kesho mjini Harare.
Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto alisema timu hiyo imeondoka na msafara wa watu 25 ambapo ni Mkuu wa msafara mmoja toka TFF,  benchi la ufundi watu sita na wachezaji 18.
‘Twiga Stars inayonolewa na kocha mkuu, Nasra Juma inaondoka ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa marudiano, baaada ya kuwa kambini kwa takribani wiki mbili kwa maandalizi ya mchezo huo,” alisema Kizuguto
Pia Kizuguto alisema kocha Nasra akishirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo wamerekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita na wana imani ya kufanya vizuri na kuweza kusonga mbele katika hatua ya pili.
Mkuu wa msafara ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake TFF, Amina Karuma, benchi la ufundi litaongozwa na kocha mkuu Nasra Juma, kocha msaidizie Elyutery Muholery, kocha msaidizi Edina Lema, daktari wa timu Anange Lwila, mtunza vifaa Esther Chaburuma na meneja wa timu Furaha Francis.
Wachezaji wanaosafiri ni Fatuma Omary, Stumai Abdallah, Maimuna Khamis, Fatuma Issa, Anastazia Katunzi, Donisia Minja, Happyness Mwaipaja, Wema Richard na Amina Bilal.
Wengine ni Asha Rashid, Mwanahamis Omary, Belina Julius, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatibu, Mwajuma Abdallah, Amina Ramadhani, Fatuma Mustafapha na Neema Kiniga.

No comments:

Post a Comment