SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam (DRFA), zimeipongeza timu ya African Lyon kwa kufanikiwa kupanda ligi kuu msimu ujao, baada ya kuwa vinara wa Kundi A katika ligi hiyo iliyomalizika juzi.
Wakizungumza na wandishi wa habari kwa nyakati tofauti, Ofisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto na Mwemyekiti wa DRFA Almas Kasongo walisema wainaitakia kila la kheri Africa Lyon katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu, kwa kujiandaa vizuri na mikiki mikiki ambayo ina jumla ya timu 16 na kila klabu kucheza michezo 30 kwa msimu, nyumbani na ugenini.
Lyon
imefikia hatua hiyo baada ya kushinda mechi 8 na kutoka sare mechi 3 kati ya
mechi 14 ilizocheza,na kuiacha nyuma pointi 2 klabu ya KMC FC iliyomaliza
katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 25.
Pia
Kasongo amezipongeza timu za Ashanti United iliyomaliza katika nafasi ya tatu
ikiwa na pointi 24, Friends Rangers iliyomaliza katika nafasi ya nne ikiwa na
pointi 23,pamoja na Polisi Dar es salaam iliyomaliza katika nafasi ya sita
ikiwa na pointi 14 zote za Dar es
salaam,kwa uthubutu wao wa kujaribu kutinga ligi kuu.
Michuano
ya ligi daraja la kwanza kwa msimu huu wa mwaka 2015/2016, ilishirikisha timu
24 zilizopangwa katika makundi matatu yenye timu nane kila kundi,huku kila
kundi likitakiwa kutoa timu moja kuingia ligi kuu.
Timu
nyingine iliyopanda ligi kuu ni pamoja na maafande wa Ruvu Shooting ya Mlandizi
ya Pwani iliyomaliza ya kwanza katika kundi “B” wakijikusanyia pointi 33, huku
katika kundi la “C” uamuzi wa TFF unasubiriwa baada ya timu za Polisi Tabora na
Geita Gold FC, kumaliza wakiwa
wamefungana pointi 30 zikiwa sawa kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
No comments:
Post a Comment