Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, February 13, 2016

LIGI KUU ENGLAND LEO ARSENAL vs LEICESTER CITY, MANCHESTER CITY vs TOTTENHAM HOTSPUR

Mechi zitakazochezwa leo baina ya timu 4 za kwanza zitaamua mwelekeo halisi wa ligi hii yenye wapenzi wengi duniani.
Arsenal itamenyana na Leicester City ambayo bado inaongoza ligi ikiizidi Arsenal alama 5.
Arsenal iko kwenye nafasi ya tatu na ushindi wake utapunguza pengo baina yake na Leicester na kuipa matumaini zaidi ya kuendelea kupigana hadi mwisho.
Nayo Manchester City yenye nafasi ya 4 itaialika Tottenham iliyo kwenye nafasi ya pili.
Bila shaka mshindi atajiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea na mbio za kuwania ubingwa.
Miongoni mwa mechi zitakazopigwa jumamosi hii ni Sunderland kupepetana na Manchester United na Everton kuzipiga na West Brom.

No comments:

Post a Comment