Nahodha wa Chelsea, John Terry anatarajiwa kuachana na klabu yake ya Chelsea baada ya timu hiyo kuonyesha nia ya kutokuhitaji kuongeza mkataba na mchezaji uyo.
john-terry-1425370038
Terry aliyejiungana Chelsea akiwa na miaka 14 aliweka wazi mipango ya klabu yake kuachana na nae na kueleza kuwa anapendelea kusalia katika klabu hiyo lakini uongozi unaonekana kutokuhitaji kuendelea nae.
“Napenda kuendelea kubaki hapa lakini uongzi wa klabu unaonekana kuwa tofauti,” alisema Terry.
Hata hivyo mmoja wa wazungumzaji wa klabu hiyo alikaririwa Jumapili akisema kuwa Terry bado hajapewa mkataba mpya na bado uongozi haujaamua hatama ya mchezaji huyo,
Terry mpaka sasa ameshaichezea Chelsea michezo 696 na amefanikiwa kushinda makombe manne ya Ligi Kuu ya Uingereza, makombe ya FA Cup mara tano na kombe moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.