SIMBA na
Azam FC na kesho na jumapili zina nafasi kubwa ya kuiengua Yanga kileleni endapo
zitashinda mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara zitakazopigwa kwenye viwanja
tofauti.
Yanga
inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 43 haitashuka dimbani wikiendi hii katika
mchezo wa ligi hiyo kwani inacheza na Cercle De Joachim Mauritius katika mchezo
wa awali wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika.
Simba na
Azam FC wako katika nafasi ya pili na tatu na wamefunga kwa pointi, ambapo kila
moja ina pointi 42 na kama zitashinda zitafikisha 45 na kuiondoa Yanga
kileleni.
Simba
ambao tangu waanze kufundishwa na Mganda Jackson Mayanja wameshinda mechi zao
zote, leo watakuwa wageni wa Stand United katika mchezo utakaofanyika kwenye
Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Stand
United wako katika nafasi ya tano na watataka kuizuia Simba na kudhihirisha
makali yao, hivyo pambano hilo linatarajiwa kuwa lenye ushindani wa hali ya juu
kutoka kwa timu hizo.
Wenzao
Azam FC nao watakuwa ugenini wakicheza na Coastal Union ya Tanga katika mchezo
utakaofanyika kesho kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Azam FC
kabla ya mchezo wa huo wako nyuma kwa mechi mbili, hivyo kama itashinda zote
itafikisha pointi 48, hivyo ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri ukilinganisha na
Simba na Yanga.
Katika
mchezo mwingine; Mgambo JKT itacheza
na kaka zao wa African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Mbeya City watakuwa
wageni wa Toto Africans, Ndanda FC dhidi
ya Majimaji.
JKT Ruvu
wataikaribisha Kagera Sugar wakati Mwadui ya Shinyanga itakuwa mwenyeji wa Tanzania
Prisons.
No comments:
Post a Comment