Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 26, 2016

Ramires wa Chelsea kusajiliwa China, dili lakaribia kukamilika

Ramires


Kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Brazil, Ramires anatarajiwa kusajiliwa na klabu ya Jiangsu Suning usajili unaotarajiwa kukamilika muda wowote kuanzia sasa.

Ramires, 28 anatarajiwa kuondoka Chelsea ambayo alijiunga  mwaka 2010 akitokea Benfica ya Ureno kwa ada ya Pauni Milioni 17 na anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo ya China kwa ada ya Pauni Milioni 25.

Oktoba mwaka jana Ramires alisaini mkataba na Chelsea wa miaka minne na sasa wana muuza Jiangsu ambayo inaongozwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Dan Petrescu na kwa msimu wa 2015 ilimaliza katika nafasi ya tisa na kufanikiwa kushinda kombe la China (Chinese Cup 2015).

Akiwa na Chelsea, Ramires alifanikiwa kushinda kombe la Ligi Kuu ya Uingereza, Kombe la FA, Capital One, kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Ligi ya Europe yote mara moja moja.

No comments:

Post a Comment