“Mimi ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Elimu ya Viungo (PE), na kwa kuondoka Yanga SC maana yake napata wasaa mzuri wa kumtumikia mwajiri wangu, UDSM,” amesema.
Pamoja na Tiboroha kutozama ndani sana juu ya kujiuzulu kwake, lakini inaelezwa alikuwa hana maelewano na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Isaac Chanji ambaye kwa sasa ndiye mtu anayesikilizwa na kuaminiwa zaidi na Manji.
Tayari Jonas Tiboroha amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti Yusuf Manji.
Mtandao huu unaendelea kufatilia zaidi juu ya kujiuzulu kwa Dr. Tiboroha na utaendelea kutoa taarifa kadiri zitakavyokua zikitokea.
No comments:
Post a Comment