adebayor-transfer-crystal-palace-social_3406133

Mshambukiaji wa zamani wa Arsenal, Manchester City na Tottenham, Emmanuel Adebayor amekamilisha usajili wa kujiunga na Crystal Palace inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza kwa mkataba  utakaomalizika msimu wa 2015/2016.
Kabla ya kusajiliwa na Crystal Palace, Adebayor alikuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo na Ijumaa ya wiki iliyopita kocha Alan Pardew alizungumza mbele ya vyombo vya habari kuwa wanatarajia kumsajili mchezaji mwenye jina kubwa ambaye wanaamini ataweza kuisaidia klabu hiyo.
Baada ya kusajiliwa Adebayor anaweza kupata nafasi ya kucheza katika mchezo wake wa kwanza wa Kombe la FA wa raundi ya nne wakati Crystal Palace itakapowakaribisha Stoke City, na Adebayor anatarajiwa kuendelea kuitumia jezi namba 25 ambayo amekuwa akiitumia katika klabu nyingi alizochezea.