Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 24, 2015

VAN GAAL AKUTANA NA WANAHABARI, AJIBU MASWALI MATATU TU NA KUONDOKA


Huku akisakamwa na uvumi wa kufukuzwa kazi, Mdachi huyo alionyesha wazi hafurahii hali hiyo na kusisitiza amekuja mbele yao kwa sababu tu ya Kanuni za Ligi Kuu England zinazoamrisha Mameneja kuongea na Wanahabari kabla ya Mechi ya Ligi na mara baada ya Mechi hizo.
Huku akitoka kwenye Chumba cha Mahojiano, Van Gaal aliwaambia Waandishi: “Nawatakia Krismasi njema na pengine Mwaka Mpya mwema tukionana. Furahieni Mvinyo na Mikate ya Nyama ya Kusaga!”

MAHOJIANO KAMILI:
Swala la 1:"Louis, asante kwa muda wako. Arsene Wenger Leo amesema uvumi kuhusu hatima yako ni utovu wa nidhamu, Je unakubaliana na hilo?

Jibu:"Hivi kuna Mtu kwenye chumba hiki hajisikii kuniomba radhi? Hakuna Mtu mwenye hisia hizo? Nashangaa kuhusu hilo!”

Swali la 2:"Tumekukosea nini?"
Jibu:"Nadhani nilikuwa nishafukuzwa kazi, nimesoma hayo…Nimefukuzwa. Mtu wa kunirithi tayari yupo!”

“Hivi mnafikiria nini kinatokea kwa Mke wangu au Watoto wangu au Wajukuu zangu au Mashabiki wa Manchester United au Marafiki zangu? Mnafikiria nini? Wamenipigia simu mara nyingi na pia Arsene Wenger amesema kitu kuhusu hilo!”

“Hivi mnafikiri nataka kuongea na Wanahabari hivi sasa? Nipo hapa kwa sababu ya Kanuni za Ligi Kuu tu. Inabidi niongee na nyinyi. Lakini ninachoona nikiongea kitu mnakichukua mnavyotaka nyinyi! Nataka kusema tu nimehamasisha kuinua imani ya Wachezaji wangu, nimefanya kila kitu wiki hii. Nimefanya Mikutano, Mikutano ya tathmini na Wachezaji wangu, na Wafanyakazi wangu, tumepata Lanchi ya Krismasi, nimetoa spichi na nimeona upendo na sapoti ya kila Mtu Carrington, hapa Kituo chetu cha Mazoezi cha Aon.”
“Lakini sioni hilo kwa Wanahabari na, ni wazi, najua mtaandika hilo. Sasa hatupo kwenye nafasi nzuri lakini Wiki 4 nyuma tulikuwa Nambari Wani kwenye Ligi na baada ya Wiki 4 tunaweza kuwa wa Kwanza tena”
Swali la 3:"Umepitia haya haya katika Klabu kubwa kabla, Klabu kubwa kabisa. Lakini hii ni Manchester United na kama matokeo hayaendi vizuri na Mashabiki wakageuka ni wazi uvumi utatokea. Hivi hushangai kuwepo uvumi?”
Jibu:"Hapana, sidhani kama mnaweza kufanya hivyo lazima mfuate ukweli na hasa wakati napigiwa Simu na Sir Alex Ferguson, David Gill na Ed Woodward kwa sababu nyie mnazua mambo yasiyo mazuri, ambayo si kweli na sasa nijibu maswali yenu!”

“Sidhani kama nataka kufanya hilo. Sasa natilia mkazo kwa Stoke City, nawasaidia Wachezaji wangu.”

“Nawatakia Krismasi njema na pengine Mwaka Mpya mwema tukionana. Furahiane Mvinyo na Mikate ya Nyama ya Kusaga! Kwaherini!”

No comments:

Post a Comment