Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 26, 2015

PELLEGRINI ASEMA MBIO ZA UBINGWA BADO


MENEJA wa Man City Maneul Pellegrini anaamini kipigo chao kutoka kwa Arsenal Jumatatu iliyopita cha 2-1 huko Emirates hakitaathiri kampeni yao ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Msimu huu.

Kipigo hicho kimewaacha Man City wakiwa Nafasi ya 3 Pointi 4 nyuma ya Arsenal ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Leicester City.
Leo Man City wapo kwao Etihad kucheza na Sunderland ambao kawaida huivimbia City wakati Leicester na Arsenal zote ziko Ugenini kwa Arsenal kucheza huko Saint Mary na Southampton na Leicester kuwa Anfield kuivaa Liverpool.
Ikiwa Leicester watatetereka na Arsenal kushinda, basi Arsenal watatwaa uongozi hii Leo.

Lakini Pellegrini anaamini City, iliyotwaa Ubingwa Mwaka 2012 na 2014, inaweza kushinda Mechi yake ya Leo na ya Jumanne Ugenini na Leicester.
Pellegrini ameeleza: “Tupo Nafasi ya 3, Pointi 4 nyuma ya Arsenal na Pointi 6 nyuma ya Leicester. Ni muhimu kushinda Mechi zetu hizi 2 za sasa tumalize Raundi ya kwanza ya Ligi tupo juu. Kitu muhimu ni kuimaliza Januari tuko juu, kisha tujaribu na kutwaa Ubingwa!”

Aliongeza: “Tumepoteza Pointi muhimu na Arsenal lakini si Gemu iliyoamua chochote. Hutwai Ubingwa Mwezi Desemba!”
Habari njema kwa Pellegrini ni kurejea Uwanjani kwa Kepteni wake Vincent Kompany ambae alikuwa Majeruhi na Msimu huu katika Mechi 8 alizocheza City haijafungwa na ilishinda Mechi 6 na kufungwa Bao 1 tu wakati kipigo cha Arsenal ni Mechi yao ya 5 kati ya 9 ambazo walifungwa bila Kompany.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZA LEO HII JUMAMOSI BOXING DAY!
Jumamosi Desemba 26

15:45 Stoke v Man United
18:00 Aston Villa v West Ham
18:00 Bournemouth v Crystal Palace
18:00 Chelsea v Watford
18:00 Liverpool v Leicester
18:00 Man City v Sunderland
18:00 Swansea v West Brom
18:00 Tottenham v Norwich
20:30 Newcastle v Everton 

22:45 Southampton v Arsenal

No comments:

Post a Comment