Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi
akimuwakilisha Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akizindua
rasmi albam mbili za kwaya ya Wakorintho wa Pili kwenye tamasha la
Krismas lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo, ambapo
mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini Rebecca
Malope amefanya onesho kubwa lililovuta hisia za mashabiki wengi
waliohudhuria katika tamasha hili akishirikiana na waimbaji mbalimbali
wa hapa nyu mbani na nchi jirani ya Kenya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
huo Nape Nnauye amewaomba watanzania kuzidi kumuombea Rais Dk . John
Pombe Magufuli kwa kazi ya kutumbua majipu ambayo amekwishaianza kwani
kazi hiyo ni ngumu na ina vikwazo vingi, lakini pia amewataka watanzania
na waumini wa madhehebu mbalimbali kuwaombea wasaidizi wake ili waweze
kuwa bega kwa bega na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kutekeleza
kazi hii kwa ufanisi na kisha watanzania wafaidi matunda na rasilimali
zao wenyewe.
Waimbaji kutoka Kenya walikuwa ni
Faustine Munishi na Sara K na Solomon Mukubwa kutoka jiji la Nairobi
huku waimbaji wa hapa nyumbani wakiwa ni Rose Muhandom Upendo Nkone,
Christine Shusho, Edson Mwasabwite, Joshua Mlelwa na wengine wengi,
Tamasha hilo pia lilikuwa na lengo la kumshukuru mungu kwa nchi yetu ya
Tanzania kufanya uchaguzi kwa amani, Kulia ni Akex Msama Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo.(PICHA NA
JOHN BUKUKU- FULLSHANGWEBLOG-DAR ES SALAAM)
Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni
ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo. akimkaribisha
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye ili
kuzungumza na wananchi katika tamasha hilo kushoto ni Mbunge Martha
Mlata na MC Mwakipesile mshereheshaji wa Tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi na mashabiki
waliohudhuria katika tamasha hilo katikati ni Akex Msama Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo na kushoto
ni MC Mwakipesile.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiimba moja ya mapambio na
kuitikiwa na mashabiki wa nyimbo za injili waliohudhuria katika tamasha
hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye pamoja na maaskofu na viongozi
mbalimbali wakishiriki katika sala maalum ya maombi iliyofanyika katika
tamasha hilo,
Wamumini na mashabiki mbalimbali
wa muziki wa injili wakishiriki katika maombi maalum ya kumshukuru mungu
yaliyofanyika kwenye tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape
Nnauye wakicheza pamoja na mwimbaji Upendo Nkone kutoka kulia ni Mbunge
Martha Mlata na Alex Msama wakishiriki kucheza.
Mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
Waimbaji wa mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
Mwimbaji Rebecca Malope akiimba kwa hisia huku meza kuu pamoja na mashabiki wake wakiwa wamesimama.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs
Rhobi Nape Nnauye pamoja na maaskofu mbalimbali wakiwa wamesimama
wakati mwimbaji Rebecca Malope akifanya vitu vyake katika tamasha
hilo.
Mwimbaji Christine Shusho na Mbunge Martha Mlata wakiimba pamoja wakati wa Tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye,Alex Msama na Mkewe na baadhi ya wabunge kulia ni Martha Mlata na kushoto ni Mary Majelwa wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya akiiimba katika tamasha hilo.
Wanakwaya wa Wakorintho wa pili wakiimba wimbo wao mara baada ya kuzinduliwa kwa albam zao katika tamasha hilo.
Mwimbajo kutoka nchini Kenya
Solomon Mukubwa akiimba na mwimbaji mwenzake kutoka kushoto Sara K.
huku mbunge Martha Mlata akishiriki kuimba nao.
Mwimbaji Joshua Mlelwa naye amefanya mambo makubwa jukwaani katika tamasha hilo.
Mwimbaji Rose Muhando pamoja na waimbaji wake wakifanya vuti vyao jukwaani.
No comments:
Post a Comment