Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 4, 2015

Mwandishi Gwiji wa habari za michezo Willie Chiwango afariki dunia

Mwandishi gwiji wa habari za michezo nchini, Willie Chiwango akizungumza katika moja ya mikutana ya wahariri wa michezo nchini. Kulia ni Mwina Kaduguda na kushoto ni Salim Salim.Mwandishi gwiji wa habari za michezo nchini Willie Chiwango amefariki dunia usiku wa kuamkia leo!
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa na Jina Lake Litukuzwe. Amina.
Chiwango wakati wa uhai wake (kushoto) akiwa na mpiga picha mashuhuri Issa Michuzi.

Willie Chiwango (kulia) akisalimiana na mwanariadha wa zamani wa Zanzibar Mosi Ally kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

 
 
Habari wadau, nasikitika kuwajulisha kuwa tumepata msiba wa mwanafamilia mwenzetu na mwanataaluma wa siku nyingi katika uandishi wa habari za michezo nchini, Willie ‘Willy’ Chiwango,
Chiwango alifariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Massana, Dar es Salaam na msiba upo nyumbani kwake Ilala Mchikichini, Dar es Salaam, ambapo mipango ya maziko inafanyika.
Wakati wa uhai wake marehemu Chiwango alifanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya serikali, Daily News na Sunday News. Pia amepata kufanya kazi This Day na vyombo vingine.
Kwa wanaohitaji taarifa za msiba huu, namba za wahusika ni mtoto wa marehemu 0659-353006, kama ukimkosa hata mjane wa marehemu pia anazungumza 0652-722173.
Naomba tushirikiane na familia katika kipindi hiki kigumu. Mungu amuweke mahali pema peponi marehemu Mzee Willy Chiwango. Amina.
Ahsanteni,
Katibu Mkuu TASWA.