Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 4, 2015

SIR ALEX FERGUSON AMMIMINIA SIFA MCHEZAJI WAKE WA ZAMANI GARY NEVILLE, ASEMA ATALETA MAENDELEO VALENCIA

Sir Alex Ferguson amemuunga mkono Mchezaji wa zamani wa Manchester United Gary Neville kufanikiwa kama Meneja mara baada ya kuteuliwa kuiongoza Valencia ya Spain hadi mwishoni mwa Msimu huu.
Neville, mwenye Miaka 40, alitumia maisha yake yote ya uchezaji Soka akiwa chini ya Sir Alex Ferguson huko Manchester United ambako alicheza Mechi 602 na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Englamnd mara 8, FA CUP mara 3, Kombe la Ligi mara 2 na UEFA CHAMPIONS LIGI wakati akiwa Mchezaji kati ya 1993 na 2011.
Sir Alex anaamini kipaji cha Gary Neville kilichompa mafanikio kama Mchezaji na pia Mchambuzi wa Soka kitamsaidia kupata mafanikio kama Meneja.
Ferguson ameeleza: “Gary ana sifa nyingi zinazoonyesha atafanikiwa kama Meneja. Umahiri kama Kiongozi, uaminifu na uchapa kazi wake. Ni Mtu ambae haogopi kufanya maamuzi makubwa na hiyo ni sifa kubwa kwa Mtu anaeongoza. Nadhani atafanya vizuri na namtakia yeye na Ndugu yake Phil, kila la heri.”

Neville, ambae pia aliichezea England mara 85, aliteuliwa kuwa Meneja mpya wa Valencia hapo Jana na Mmiliki wa Klabu hiyo ya La Liga Peter Lim ambae ni Tajiri kutoka Singapore ambae pia ni Rafiki wa Neville.
Uteuzi huo ulimfanya Neville ajiuzulu kama Mchambuzi wa Sky Sports lakini atabaki kama Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya England chini ya Roy Hodgson.
Baada ya kujiuzulu kwa Kocha Nuno Wikiendi iliyopita baada ya kufungwa 1-0 kwenye La Liga na Sevilla na kutupwa Nafasi ya 9, Valencia iliwekwa chini ya uongozi wa muda wa Phil Neville, mdogo wa Gary Neville ambae aliteuliwa kama Meneja Msaidizi tangu Julai, pamoja na Voro, ambae ndie kaimu Meneja.
Jana Voro na Phil Nevill waliiongoza Valencia kuifunga Barakaldo 3-1 kwenye Copa del Rey na pia wataendelea kuiongoza Jumamosi itakapopambana na Barcelona kwenye La Liga.
Mechi ya kwanza ya Valencia chini ya Gary Neville itakuwa Desemba 9 dhidi ya Lyon ikiwa ni Mechi ya Kundi H la UEFA CHAMPIONS LIGI.