Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 18, 2015

MAN UNITED IPO KWENYE NAFASI YA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, HISTORIA INAWALINDA

Wachambuzi na wadodosaji wa Takwimu za Soka wameibuka na kudai kuwa Manchester United inaweza kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu.
Hivi sasa, Man United, chini ya Meneja Louis van Gaal ambae ameshaanza kukumbwa na manung’uniko ya Washabiki, wapo kwenye wimbi la Mechi 5 bila ushindi.
Mara ya mwisho Man United kushinda ni Novemba 21 walipoifunga Watford 2-1 kwa Bao la ushindi la kujifunga mwenyewe Troy Deeney katika Dakika ya mwisho ya Gemu hiyo.

Baada ya hapo, Man United walitoka Sare na PSV Eindhoven katika UEFA CHAMPIONS LIGI na kufuatia Sare za Ligi na Leicester City na West Ham na kisha kufungwa na Wolfsburg kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI na kufuatia kipigo cha Wiki iliyopita kutoka kwa Bournemouth kwenye Ligi.


DONDOO MUHIMU:
-Man United wameifunga Norwich kwa Bao 4-0 katika Mechi 3 zilizopita zilizochezwa Old Trafford.
-Mechi hizo ni Ligi Kuu England, Machi 2013, Ligi Cup Oktoba 2013 na Ligi, Aprili 2014.

Lakini, licha ya tafrani hiyo yote kwa Man United na Mashabiki wake, na hata kama hawatashinda Jumamosi dhidi ya Norwich City kwenye Mechi ya Ligi Uwanjani Old Trafford na kuendeleza wimbi la kutoshinda kufikia Mechi 6, Historia bado inawasapoti Man United kuweza kutwaa Ubingwa. Mara ya mwisho kwa Man United kwenda Mechi 6 mfululizo bila ushindi katika Mashindano yote walifanikiwa Msimu huo huo kutwaa Ubingwa wa England na hiyo ni Msimu wa 1992/93 na ule Msimu unaokumbukwa sana wa 1998/99 walipotwaa Trebo kwa kuzoa Ubingwa wa Ligi Kuu England, FA CUP na UEFA CHAMPIONS LIGI.
Mwaka 1996 pia walitwaa Ubingwa baada ya Msimu huo kwenda Mechi 5 mfululizo bila ushindi katika Mechi za Ligi.
Mara zote hizo 3, Man United ilikuwa chini ya Meneja Lejendari Sir Alex Ferguson alietwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 13 kwenye Misimu ya 1992–93, 1993–94, 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11 na 2012–13.
Wanatakwimu wamedai wimbi la sasa pia haliwezi kuwaathiri kwa vile Timu zinapoteza Pointi kila kukicha na wao bado wapo nafasi nzuri wapo Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Leicester, 4 nyuma ya Timu ya Pili Arsenal na 3 nyuma ya Timu ya 3 Man City.
Mechi zinazofuata kwa wikiendi  ni Leicester kucheza Ugenini na Everton na Arsenal kuikaribisha Man City huko Emirates.