Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 12, 2015

DROO YA FAINALI EURO 2016 KUFANYIKA LEO

DROO ya kupanga Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, itafanyika leo  Desemba 12 huko Paris Nchini France ambako Fainali hizo zitafanyika.
Droo hiyo itakuwa na Timu 24 ambazo zimegawanywa katika Vyungu Vinne vyenye Timu 6 kila kimoja kulingana na Nafasi zao za kwenye Listi ya Ubora.

Fainali za EURO 2016 zitachezwa Mwakani kuanzia Juni 10 hadi Julai 10 huko France.
DROO-Mgawanyo wa Vyungu:
Kila Chungu kitatoa Timu 1 kuingizwa kwenye moja ya Makundi 6 [A hadi F]
France, kama Wenyeji, wao wapo Kundi A

CHUNGU A
France, Germany, Spain, Portugal, Belgium, England

CHUNGU B
Italy, Austria, Switzerland, Russia, Croatia, Ukraine

CHUNGU C
Czech Republic, Sweden, Poland, Romania, Slovakia, Hungary

CHUNGU D
Turkey, Republic of Ireland, Iceland, Wales, Albania, Northern Ireland


TIMU ZILIVYOFUZU:
-France [Wenyeji]
-KUNDI A: Iceland, Czech Republic, Turkey
-KUDI B: Belgium, Wales
-KUNDI C: Spain, Slovakia
-KUNDI D: Germany, Poland
-KUNDI E: England, Switzerland
-KUNDI F: Northern Ireland, Romania
-KUNDI G: Austria, Russia
-KUNDI H: Italy, Croatia
-KUNDI I: Portugal, Albania
-Mechi za Mchujo: Hungary, Ireland, Ukraine, Sweden

Fainali zitafanyika lini:
Euro 2016 itaanza Ijumaa Juni 10 na kumalizika Jumapili Julai 10.
Hii ni mara ya kwanza kwa Fainali hizi kuwa na Timu 24 na hivyo itakuwepo Raundi ya Mtoano ya Timu 16, kisha Robo Fainali na Nusu Fainali.

Viwanja vya Mechi za Fainali:

Euro 2016 itatumia Viwanja 10 Nchini France:

Stade de Bordeaux, Bordeaux (Watu 42,000)

Stade Bollaert Delelis, Lens Agglo (35,000)

Stade Pierre Mauroy, Lille Metropole (50,100)

Stade de Lyon, Lyon (58,000)

Stade Velodrome, Marseilles (67,000)

Stade de Nice, Nice (35,000)

Parc des Princes, Paris (45,000)

Stade de France, Saint-Denis (80,000)

Stade Geoffroy Guichard, Saint-Etienne (41,500)

Stadium de Toulouse, Toulouse (33,000)

**Fainali itachezwa Stade de France