Tuesday, December 15, 2015
SAMATTA ATINGA FAINALI KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA
Star wa TP Mazembe na Tanzania Mbwana Ally Samatta ameingia kwenye headlines nyingine Afrika baada ya jina lake kutinga kwenye fainali za wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika 2015.
Samatta yuko katika nafasi nzuri ya kutwaa tuzo hiyo baada ya kuibuka mfungaji bora wa michuano ya klabu bingwa Afrika na kuisaidia timu yake kutwaa taji hilo kubwa barani Afrika kwa upande wa vilabu.
Majina ya wachezaji walioingia fainali kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2015 yametajwa leo jijini Abuja, Nigeria mbele ya waandishi wa habari.
Wachezaji watatu walioingia kwenye fainali ya tuzo ya mchezaji bora wa Afrika (kwa ujumla) ni kama ifuatavyo;
Andre Ayew (Ghana/ Swansea City-England), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon/ Burussia Dortmund-Ujerumani) na Yaya Toure (Ivory Coast/ Manchester City-England).
Majina ya wachezaji wa wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wanaocheza ligi za ndani (vilabu vya Afrika) ni pamoja na;
Baghdad Boundjah (Algeria/ Etoile du Sahel-Tunisia), Mbwana Ally Samatta (Tanzania/ TP Mazembe-Congo DR), na Robert Kidiaba (DRC/ TP Mazembe-Congo DR).
Washindi wa tuzo hizo watapatikana kwa kupigiwa kura na makocha wa kuu wa timu za taifa pamoja na wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya soka vya nchi wanachama wa CAF.
Sherehe za kuwatangaza na kuwakabidhi washindi wa tuzo hizo zitafanyika January 7, 2016 nchini Nigeria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment