Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 31, 2015

Barcelona yavunja rekodi ya Real Madrid, ipo hapa

2341052_heroa

 


Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania imefanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa na wapinzani wao wakubwa Real Madrid ambayo waliiweka mwaka 2014.
Real Madrid mwaka jana ilifanikiwa kufunga magoli 178 ambayo yalikuwa hayajawahi kufungwa na klabu yoyote katika historia ya klabu ya Hispania.
Awali kabla ya mchezo kati ya Barcelona na Real Betis, Barcelona ilikuwa na magoli 176 na baada ya kuibuka na ushindi wa goli nne kwa bila dhidi ya Real Betis sasa Barcelona ndiyo timu inayoongoza kwa kufunga magoli mengi kwa mwaka mmoja kwa kuwa na magoli 180 na kuiacha Real Madrid ikiwa na magoli 178.
Kati ya magoli 180, Lionel Messi amefunga magoli 48, Suarez 48 na Neymar 41 ambayo ni sawa na asilimia 75 ya magoli yote ambayo Barcelona imefunga.
Aidha katika mchezo huo, mchezaji bora wa dunia mara nne, Lionel Messi alifanikiwa kufikisha michezo 500 akiichezea Barcelona.