Kocha wa Leicester City, Claudio Ranieri (pichani) amesema bado hawawezi kubashiri kama wanaweza kuibuka mabingwa wa Ligi Kuu ya Wingereza na hakuna anayewaza hilo ndani ya kikosi chake.
Ranieli
ameyasema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi ya Uingereza kati
ya Leicester City iliyowakaribisha Manchester City ambapo mchezo huo
ulimalizika kwa sare ya bila kufunguna kwa timu hizo.
Alisema
kuwa ligi ya Wingereza imekuwa haitabiriki unaweza kuwa katika kiwango
kizuri lakini hali ikabadilika na nafasi ikachukuliwa na timu nyingine
ambayo akafanikiwa na kuchukua ubingwa.
“Hii
ligi inashangaza sana, nadhani timu kubwa zinaweza kuwa katika kiwango
cha juu lakini muda mwingine hakuna mtu anataka kushinda ligi, mambo
yanabadilika katika ligi hii,
“Sio rahisi kwetu lakini tunataka kupambana na kila mtu, ni maajabu haya tunayoyafanya,” alisema Ranieli.
Aidha
Ranieli amesema anaridhishwa na kasi waliyonayo wachezaji wake na kwake
limekuwa jambo la kushangaza kutokana na kasi waliyonayo na anatumai
kuwa kasi hiyo itaendelea kuwepo na watafika mbali zaidi.
Leicester
kwa sasa wamefikisha alama 40 wakiwa katika nafasi ya pili nyuma ya
Arsenal ambao wanalingana nao alama na Arsenal ikiwa imewashinda
Leicester magoli ya kufungwa na kufunga.
Msimu
uliopita hadi kumaliika kwa mwaka 2014 kuingia 2015, Leicester City
ilikuwa katika nafasi ya mwisho ya msimamo wa Ligi Kuu ya Wingereza
lakini kunaonekana kuwapo na mabadiliko makubwa katika klabu hiyo baada
ya kumchukua Ranieli kuwa meneja wa klabu na sasa inaonekana kuwa na
mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment