TAMASHA la
kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo linatarajiwa kufanyika kwa mara ya 34
kuanzia Septemba 21-27, katika ukumbi waTaasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
ambao ndio wenyeji na waandaaji wa tamasha hilo kongwe Tanzania
Akizungumza
jijini jana, Mwenyekiti wa Tamasha hilo, John Mponda Lengo tamasha hilo liliasisiwa mwaka 1981 na
Chuo cha Sanaa, Bagamoyo ambacho kwa sasa ni Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo ni kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cha sanaa kuonyesha kwa vitendo
yale waliojifunza kwa mwaka mzima kwa kuwashirikisha wakazi wa Bagamoyo.
“Tamasha
lina lengo la kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cha sanaa kuonyesha kwa vitendo
yale waliojifunza wakati wakiwa chuoni kwa kuwashirikisha wakazi wa Bagamoyo na
limebeba kauli mbiu inayosema ‘SANAA NA UTAMADUNI KATIKA UCHAGUZI HURU NA WA
AMANI’”, alisema Mponda.
Pia alisema Vikundi
mbalimbali vya ndani na nje ya nchi zitashiriki ili kubadilishana Uzoefu pia
litahusisha Ngoma za Asili, Maigizo, Sarakasi, Mazingaombwe, Muziki wa kisasa
na asili, Sanaa za Ufundi na bidhaa mbalimbali.
Mponda alisema kutatolewa mada ndogondogo kupitia kongamano na warsha zitakazohusu Haki za binadamu, Rushwa na kupinga Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)
Jumla ya vikundi 48 kutoka ndani na nje ya Tanzania vimethibitisha kushiriki,ambapo vikundi 43 ni kutoka ndani ya Tanzania na vikundi 5 kutoka nchi za Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Korea na Congo.

Mponda alimaliza kwa kuomba udhamini kwa wadau mbalimbali wa sanaa, makampuni,Taasisi za serikali na zisizo za serikali kujitokeza kudhamini tamasha hili muhimu kwa mustakabali wa sanaa na utamaduni wa Mtanzania.
No comments:
Post a Comment