BONDIA Lulu
Kayage ameibuka kidedea baada ya kumpiga wa KO bondia Lizbeth
Sivhaga wa Afrika Kusini.
Pambano hilo
lilifanyika juzi kwenye mji wa Limpopo ni pambano la kwanza kwa Lulu kucheza
nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa K.O katika raundi ya pili.
Akizungumza baada ya kuwasili nchini, Rais wa
TPBO, Yasin Ustaadhi Abdallah ambaye alambatana na bondia huyo, alisema kuwa
mchezo huo ulioanza kwa kasi huku kila mmoja akionesha mashambulizi kutaka
kumpiga mwenzie katika raundi za awali.
“Pambano
lilikuwa zuri kwani kila mmoja akionesha nia ya kumpiga mwenzake lakini ilivyofika
raundi ya pili bondia Lulu alimwelemea sana mpinzani wake kwa makonde mfululizo
na wasaidizi wake kumuokoa kwa kumtupia taulo hivyo Lulu alishinda K.O ya
raundi ya pili”, alisema Yasin.
Pia Yasin
alisema bondia Ramadhani Shauri amepoteza pambano wake kwa kupigwa K.O ya
raundi ya nne na bondia Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini, pambano ambao
ulikuwa wa raundi nane.
Naye bondia
Lulu amewashukuru watanzania kwa dua zao kwani haikuwa kazi rahisi kupambana na
kushinda ukiwa ugenini, pia alimshukuru kocha wake Habibu Kinyogoli kwa mbinu
ambazo amekuwa akimpa hadi kufikia hapo alipo.
No comments:
Post a Comment