Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa
Morogoro (MRFA) jana kilifanya uchaguzi wa viongozi wake katika nafasi ya
mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu, mweka hazina, mjumbe wa mkutano mkuu
pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
Katika uchaguzi huo Paschal Kihanga
aliibuka na ushindi katika nafasi ya mwenyekiti, huku Gracian Max Makota akishinda nafasi ya makamu mwneyekiti, nafasi
ya katibu mkuu imechukuliwa na Charles Mwakambaya na katibu msaidizi Jimmy
Lengme.
Nafasi ya Mweka Hazina imechukuliwa
na Peter Mshigati, Mjumbe wa mkutano mkuu ni Hassan Mamba na mwakilishi wa
vilabu ni Ramadhani Wagala, Kamati ya utendaji wamechaguliwa Mrisho Javu,
Rajabu Kiwanga na Boniface Kiwale.
TFF inawapongeza viongozi wapya
waliochaguliwa kuongoza chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) na kuahidi
kuendelea kushirikiana nao katika kazi za kila siku za maendeleo ya mpira wa
miguu nchini.
No comments:
Post a Comment