KLABU ya
Azam imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Allan Wanga kwa mkataba wa
mwaka mmoja.
Wanga
amejiunga Azam akitokea El Merreikh ya Sudan amesaini mktaba wa mwaka mmoja
Usajili wa Wanga unakamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni Azam FC kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Wengine ni Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ kutoka APR ya Rwanda na Serge Wawa Pascal, Kipre Michael Balou, Kipre Tchetche wote wa Ivory Coast, Brian Majwega wa Uganda na Didier Kavumbangu wa Burundi, ambao wote walikuwepo tangu msimu uliopita.
Wanga aliyezaliwa Novemba 26, mwaka 1985 mjini Kisumu, Kenya pamoja na kusaini Azam FC, lakini ndoto zake bado ni kucheza Ulaya.

Hata hatacheza
michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la kagame kwa sababu
hakuingizwa kwenye orodha ya wachezaji 20 wa Azam FC kwa ajili ya michuano
hiyo.
Picha kwa hisani ya Bin Zuberi
No comments:
Post a Comment