Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, May 16, 2015

YANGA KUMSHITAKI KASWAHILI KWA KUJIPA UONGOZI NA KUTANGAZA UCHAGUZI FEKI


Katibu Mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroha akizungumza na waandishi wa habari


UONGOZI wa Yanga umesema una sababu nne za kumshitaki kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mahakamani Francis Kaswahili kwa kutangaza katika vyombo vya habari uchaguzi ili hali yeye si kiongozi wa Yanga.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu Mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroha, alisema Mei 14 Kaswahili alitangaza uchaguzi na mchakato wake kinyume na katiba ya Yanga kwa sababu yeye si kiongozi pia si mwanachama kwa sababu mara ya mwisho kulipa ada ni 2012.
“Kisheria Kaswahili si mwanachama kwani tangu 2012 hajalipa ada na kisheria usipolipa ada uanachama unakufa na unapaswa kuomba upya”, alisema Tiboroha.
Pia alisema Yanga wanamshtaki kwa makosa ya kuchochea na kuharibu utulivu ndani ya klabu kwa kuitisha uchaguzi ikiwa ni batili na si kiongozi wa kamati ya uchaguzi wa Yanga
Kosa la pili ni kuidhalilisha klabu ya Yanga kwa kutumia jina lake kwa kujiita katibu wa kamati ya uchaguzi wa klabu wakati akijua dhahiri yeye si kiongozi katika kamati yoyote pia si mwanachama hai wa Yanga.
Tatu kuongea mambo ya uongozi wa Yanga bila kuwasiliana na Sekretarieti ya Yanga  na mwisho kutapeli wanachama wa Yanga kwa kutangaza bei ya fomu za uchaguzi bila maelekezo ya uongozi wa Yanga kuwa na taarifa.
Tiboroha alisema Yanga ina uongozi uliochaguliwa kihalali wenye mamlaka kisheria na kikatiba kupanga na kutangaza mambo yake na si vinginenvyo lakini pia akasikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari ambayo haikukamilika.
“Gazeti moja ambalo limeandika habari hizo tumeanza mchakato wa kulipeleka mahakamani na tunatafuta sauti zote zilizotangazwa na kila chombo cha habari ili kuvichukuliwa hatua za kisheria kwani Yanga ipo wazi kuongea na waandishi aidha kwa kunipigia mimi simu au Jerry Muro ambaye ni Mkurungezi wa Mawasiliano wa klabu”, alisema Tiboroha.
Aidha Tiboroha alisema walimwandikia Kaswahili barua juzi ya kumtaka kukanusha taarifa alizotangaza kupitia vyombo vya habari hadi jana saa sita mchana lakini hakutekeleza ndo maana wameamua kumpeleka kwenye kamati ya maadili na kumfungulia mashitaka ya jinai na madai dhidi yake kwa gharama zake mwenyewe.

No comments:

Post a Comment