Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, May 16, 2015

HATUJAPA OFA YOYOTE INAYOMHUSU MSUVA-YANGA



 
UONGOZI wa Yanga umekanusha uvumi ulionea kuwa umemzuia Mshambuliaji Simon Msuva kwenda kucheza soka nchini Afrika Kusini.
Akizungumzia sakata hilo katibu Mkuu wa Yanga , Jonas Tiboroha alisema kuwa Yanga haijapata ofa yoyote inayomhusu Msuva ndo maana wamekuwa kimya lakini wanashangazwa na taarifa zilizoenea kuwa wamemzuia.
“Kwanza napenda ifahamike Msuva alitoroka kwenda Afrika Kusini wakati timu ikiendelea kucheza ligi na akijua wazi yeye bado ni mchezaji wa Yanga kwani ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu hivyo nasema alijipeleka mwenyewe”, alisema Tiboroha
Aidha Tiboroha alisema wao hawana kizuizi chochote cha kumwachia mchezaji yeyete kwenda kujaribiwa akipata ofa ambayo klabu au wakala wake atafuata taratibu kwani wanajua atakapofuzu lazima klabu husika itawasiliana nao au wakishindwana wanafuata taratibi zingine ikiwa ni pamoja na kwenda FIFA.
Tiboroha alisema mpaka sasa kuna mcghezaji mmoja tu ambaye amewasilisha barua kwao ya kwenda kufanya majaribio na yupo tayari kumpa kibali lakini hakumtaja.
Amewataka wachezaji kuongeza thamani yao na utu kwa kusubiri kuitwa na si kujipeleka kwani ndo maana wanapata ofa ndogo tofauti na thamani yao.
Simon Msuva aliondoka kwenda kufanya majabio na klabu Bidvest Wits ya Afrika Kusini na amesharejea nchini na kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ambayo nayo imekwenda kwenye mashindano ya COSAFA yanayoanza leo nchini Afrika Kusini
Msuva alisajiliwa na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea Moro United, amechukua tuzo ya ufungaji bora kwani alifunga mabao 17 sawa  na Amissi Tambwe aliyefunga 17.
Endapo Msuva angefanikiwa kujiunga na Bidvest, angekuwa mchezaji wa pili wa kutegemewa na Yanga aliyeshiriki kikamilifu kuipa ubingwa msimu huu kuondoka kwani wa kwanza ni Mrisho Ngassa anayetimkia Free State Stars ya Afrika Kusini pia.

No comments:

Post a Comment