Pichani wakati wa tuzo za watu ilivyokuwa baada ya washindi kukabidhiwa tuzo zao..
Hatimaye
usiku wa Mei 22 Tanzania iliandika historia nyingine kwa kushuhudia
utoaji wa tuzo maalum zijulikanazo kama TUZO ZA WATU 2015, zilizofanyika
jijini Dar es Salaam.
Washindi
hao ni katika vipengele 13 vya mwaka huu. Majina hayo ya washindi
yaliingia baada ya kuvuka michujo miwili migumu. Ni kura za mashabiki
peke yake ndio ziliwaingiza kwenye fainali hiyo na mshindi aliweza
kupatikana kwa kura za wananchi , kama alivyonukuliwa mwenyekiti
Mtendaji wa Bongo5 Music Group, Luca Neghesti.
Washndi wa tuzo hizo za watu 2015 ni:
Mtangazaji wa redio anayependwa- D’Jaro Arungu – TBC FM.
Kipindi cha redio kinachopendwa- Papaso – TBC FM.
Mtangazaji wa runinga anayependwa– Salim Kikeke (BBC Swahili)
Kipindi cha runinga kinachopendwa- Mkasi (EATV)
Blog/Website inayopendwa- millardayo.com
Muongozaji wa video anayependwa- Hanscana
Muongozaji wa filamu anayependwa- Vincent ‘Ray’ Kigosi
Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa- Wema Sepetu
Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa- Hemedy PHD
Mwanamuziki wa kike anayependwa- Lady Jaydee
Mwanamuziki wa kiume anayependwa- Ali Kiba
Filamu inayopendwa- Kigodoro
Video ya muziki inayopendwa- ‘Nani kama Mama’– Christian Bella Feat. Ommy Dimpoz
Baadhi
ya washindi wakiwa na tuzo zao, kutoka kushoto ni Msanii bora wa kike,
Lady Jaydee akifuatiwa naa Ommy Dimpoz. anayefuata ni dada wa
mwanamuziki Ali Kiba aliyempokelea tuzo kwa niaba yake akifautiwa na
Millard Ayo.
mwenyekiti
Mtendaji wa Bongo5 Music Group, Luca Neghesti ambao ndio waandaji wa
tuzo hizo akielezea machache kwenye redcarpet juu ya tuzo hizo na kituo
cha About Bongo.com ambao ni Online TV.
‘crew friends’ marafiki KN na NS wakiwa pamoja na marafiki zao katika redcarpet katika tukio la utoaji wa tuzo za watu 2015
Mtangazaji
wa radio ya Taifa ya TBC FM, Djaro Alungu ambaye aliibuka na tuzo mbili
kwa mwaka huu na kuvunja rekodi ya aliyekuwa mtangazaji mwenzake,
Millard Ayo, akiwa na tuzo zake pamoja na crew yake.
Mtangazaji wa BBC SWAHILI, wa Dira ya Dunia, Salm Kikeke akitoa nasaha kwa waliofika wakati wa kupokea tuzo yake hiyo,
Mwanamuziki
Ommy Dimpoz akiwa katika pozi na Andrew Chale, Mwandishi Mwandamizi wa
Mtandao huu wa Modewjiblog.com muda mfupi baada ya kupokea tuzo yake.
Baadhi
ya warembo waliopamba usiku huo wa tuzo za watu 2015 chini ya
usimamizi wa Ally Rehmtullah (katikati) wakiwa katika pozi..
No comments:
Post a Comment