Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala pamoja na viongozi mbalimbali wa meza kuu kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 wakipiga picha na baadhi ya washindi wa Tuzo za Filamu 2015 jana Mei 23, zilizofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini
SERIKALI
imesema itaendelea kuweka mfumo mzuri na kujenga mazingira mazuri ili
kuhakikisha biashara ya filamu inaimarika, ikiwa ni pamoja na kuwavutia
wawekezaji binafsi waliopo tayari kuwekeza katika tasnia ya filamu.
Kauli
hiyo imetolewa jana Mei 23, jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi wa
Tuzo za Filamu 2015, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk.
Fenela Mukangala alipokuwa akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo
za filamu. Dk. Mukangala alipongeza juhudi za baadhi ya wafanyabiashara
wa filamu na wasambazaji ya kudhibiti uharamia wa kazi za filamu,
lakini aliwataka kuifanya kazi hiyo kwa manufaa ya wadau wote na sio kwa
manufaa binafsi.
“…Serikali
itaendelea kuhakikisha kwamba mazingira ya kufanya biashara ya filamu
yanaimarishwa. Pamoja na hayo ni vyema wasambazaji na wafanya biashara
wengine wa filamu wenye uwezo wakaepuka kulidhibiti soko la filamu kwa
nanufaa yao binafsi ili kujenga ushindani sawa,” alisema Dk. Mukangala.
Aliwataka wasanii na wadau wote wa filamu kuhakikisha wanaboresha kazi
zao zaidi na kufuata vigezo vinavyotambulika ili kuzitangaza kazi zao
hata nje ya nchi.
“Napenda
mtambue kuwa ubora wa bidhaa za filamu ni moja ya vigezo vya kuwa na
soko bora la filamu, kwani filamu bora hujitangaza zenyewe. Tuhakikishe
kuwa tunaongeza weledi na ubunifu. Hivi ndivyo vigezo vilivyoifanya
sekta ya filamu nchi zilizoendelea kufika hapo ilipo,” aslisema Waziri
Dk. Mukangala.
Kwa
upande wake, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA), Simon
Mwakifwamba aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kujenga chuo
maalumu kwa ajili ya filamu ili kuijengea uwezo zaidi tasnia kwani
inamchango mkubwa katika kuzalisha nafasi za ajira kwa makundi anuai.
Waliojishindia
tuzo za filamu kwa mwaka huu ‘Tanzania Film Awards 2015 (TAFA)’ katika
vipengele mbalimbali ni pamoja na Irine Sanga (Best Screen Play), Hassan
Muya (Best Actor Supporting Role), Grace Mapunda (Best Actress
Supporting Role), Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian), Irene Paul
(Best Actress), John Kalage (Best Director) na wengineo.
Tuzo
hizi kubwa ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam
katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere International Conference Center.
Zimewezeshwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, TRA,
EATV na EAR, International Eye Hospital, Foreplan Clinic, R&R
Associates, Simu Tv na Barazani Production.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala akitoa
shukrani baada ya kupokea tuzo aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na
Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA) kwenye hafla ya Tuzo za Filamu
2015.
Mama
yake na Steven Kanumba akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya
mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.Irene Paul (Best Actress) akipokea tuzo yake na Dk.Mwaka, kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015.
Irene
Paul (Best Actress)(shoto) akipongezwa na Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala kwenye hafla ya Tuzo za
Filamu 2015
Mama
yake na Steven Kanumba akipokea tuzo ya mchango mkubwa kwenye filamu
aliyotwaa mwanaye (marehemu Kanumba) kwenye tuzo za Filamu 2015.
John Kalage (Best Director) (shoto) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015
.
Hassan
Muya (Best Actor Supporting Role) (shoto) akipeana mkono na viongozi wa
meza kuu wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo yake kwenye hafla ya
Tuzo za Filamu 2015 Grace
Mapunda (Best Actress Supporting Role) akipeana mkono na Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya
kupokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015. Hassan
Muya (Best Actor Supporting Role) akipokea tuzo kwa niaba ya msanii
mwenzake Amri Athuman-King Majuto kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015
Mwakilishi
wa Mzee Jangala (Best Comedian Tanzania Film Awards 2015) akipeana
mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela
Mukangala mara baada ya kupokea tuzo kwenye Tuzo za Filamu 2015.
No comments:
Post a Comment