Wakati Meneja wa Manchester United Louis van Gaal akiwa na matumaini Kipa wake David De Gea atabakia huku akiwindwa na Real Madrid baada ya kusita kusaini Mkataba mpya ulioboreshwa aliopewa na Man United, Meneja Van Gaal amesema: "Bado naamini David De Gea atabaki!"
Licha ya kuumia na kutolewa nje ya Uwanja wakati Man United inatoka Sare 1-1 na Arsenal kwenye Mechi ya Ligi Jumapili iliyopita, Kipa huyo huenda akaanza Mechi yao ya mwisho ya Ligi watakayocheza Ugenini huko KC Stadium dhidi ya Hull City hapo Jumapili.
Kwa Man United Mechi hii ni ya kukamilisha Ratiba tu kwani washaikamata Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England lakini kwa Hull City ni lazima washinde ili kuweka hai matumaini yao kubaki Ligi Kuu England. Baada ya kutolewa kwa De Gea kwenye Mechi hiyo na Arsenal, nafasi yake ilichukuliwa na Kipa wa zamani wa Barcelona na Spain, Victor Valdes, mwenye Miaka 33, ambae alisainiwa Januari Mwaka huu
No comments:
Post a Comment