Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 9, 2018

BMT LATOA UFAFANUZI NAMNA YA KUKATA RUFAA

BARAZA la Michezo nchini (BMT) limesema shughuli za Michezo nchini zinafanyika kwa mujibu wa sheria ya Baraza la Michezo la Taifa namba 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake ya sheria namba 6 ya mwaka 1971.
Hayo yamesemwa jana na Ofisa habari wa BMT, Frank Mgunga, na kuongeza kila chama, shirikisho, klabu au asasi na taasisi zina miongozo mbalimbali inayosaidia kuendesha michezo katika maeneo yao.
“Katika kutekeleza shughuli za michezo kama mashindano, yamekuwa yakiibuka malalamiko au migogoro ambayo kwa namna moja au nyingine inahitaji utatuzi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu stahiki hasa kwa vyama vilivyosajiliwa,” alisema Mgunga
Mgunga alisema zipo taratibu za kufuata katika kuwasilisha malalamiko Malalamiko au rufaa na Mchezaji, Kiongozi, Chama, Klabu, Mwalimu, Mwamuzi, Daktari wa Timu  au mdau mwingine wa michezo anao uhuru na haki ya kuwasilisha malalamiko yake kwa kufuata utaratibu kwa ngazi ya juu endapo hakuridhika na uamuzi uliotolewa na Uongozi wa Ngazi husika.
“Malalamiko yatapelekwa kwa Chama cha Mchezo husika na kwa mujibu wa Kanuni za mchezo husika na nakala yake itapelekwa katika Kamati ya Michezo ya Wilaya katika muda usiozidi siku tatu baada ya uamuzi kutolewa,” alisema Mgunga
Pia alisema kama mlalamikaji hataridhika atakata rufaa kwa Kamati ya Nidhamu, Rufaa na Usuluhishi ngazi ya Wilaya katika muda usiozidi siku saba na kama hataridhika na uamuzi atakata rufaa kwa Kamati ya Michezo ya Mkoa katika muda usiozidi siku saba
Aidha endapo hataridhika na uamuzi wa Baraza atakuwa na haki ya kukata rufaa kwa Waziri katika muda wa siku saba na maamuzi ya Waziri yatakuwa ya mwisho.


Katika Ngazi Mkoa na Taifa  utaratibu utafuata mtiririko wa ngazi ya wilaya kupata haki hivyo Vyama vyote, mashirikisho na klabu na wadau wa michezo mnasisitizwa kufuata utaratibu huu ambao ni muhimu ili kutoruka ngazi katika kuimarisha Utawala Bora.

No comments:

Post a Comment