Mkoa
wa Kagera umeanza rasmi mashindano ya UMISETA yanayowashirikisha
wanafunzi wa shule za sekondari kutoka katika Halmashauri zote za Wilaya
na Manispaa ya Bukoba katika mkoa wa Kagera.
Mashindano hayo yalifunguliwa jana tarehe 21/05/2015 na Afisa Elimu Mkoa wa Kagera Bw. Aloyce Kamamba katika viwanja vya Chuo cha ualimu Katoke Wilayani Muleba.
Akifungua
mashindano hayo Bw. Kamamba aliwaasa wanafunzi wanamichezo ambao
wamejumuika katika chuo cha Katoke kwa kushindana katika michezo
mbalimbali kutumia fursa hiyo kuonesha vipaji vyao kwani kwa sasa
michezo ni ajira.
Pia
Bw. Kamamba aliwaasa wanamichezo hao kuhakikisha wanacheza na
kushindana kirafiki bila kucheza kwa kuumizana na kuhakikisha waamuzi
wanachezesha bila upendeleo.
Walimu
wanaohusika kuchezesha na kusimamia michezo hiyo katika mashindano hayo
ya UMISETA mkoa pia nao walihaswa kuhakikisha wanasimamia nidhamu na
kuhakikisha wanachagua wachezaji wazuri ambao watakwenda kushindana na
kuonyesha vipaji vyao pia kuleta makombe ya ushindi.
Aidha, Afisa Michezo wa Mkoa wa Kagera Bw. Kepha Elias akitoa ratiba ya mashindo alisema kuwa mara baada ya mashindano hayo kukamilika ngazi ya mkoa timu zitakazokuwa zimechaguliwa zitapiga Kambi kwa siku tatu ili kufanya maadnalizi ya kushiriki mashindano ya Kanda.
Bw. Kepha alisema kuwa mshindano ya Kanda yatafanyika mkoani Geita ambapo mara baada ya hapo wachezaji watakaokuwa wamechaguliwa wataelekea mkoani Mwanza kushiriki mashindano ya UMISETA kitaifa mkoani humo.
Mashindano hayo yalifunguliwa jana tarehe 21/05/2015 na Afisa Elimu Mkoa wa Kagera Bw. Aloyce Kamamba katika viwanja vya Chuo cha ualimu Katoke Wilayani Muleba.
Aidha, Afisa Michezo wa Mkoa wa Kagera Bw. Kepha Elias akitoa ratiba ya mashindo alisema kuwa mara baada ya mashindano hayo kukamilika ngazi ya mkoa timu zitakazokuwa zimechaguliwa zitapiga Kambi kwa siku tatu ili kufanya maadnalizi ya kushiriki mashindano ya Kanda.
Bw. Kepha alisema kuwa mshindano ya Kanda yatafanyika mkoani Geita ambapo mara baada ya hapo wachezaji watakaokuwa wamechaguliwa wataelekea mkoani Mwanza kushiriki mashindano ya UMISETA kitaifa mkoani humo.
No comments:
Post a Comment