Usaili
wa waombaji uteuzi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) unaendelea na unatarajia
kukamilika leo .
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni ilianza
usaili juzi (Agosti 30 mwaka huu) ambapo matokeo ya usaili yanatarajiwa
kutangazwa Septemba 3 mwaka huu.
Kati
ya Septemba 4 na 6 mwaka huu, Kamati ya Uchaguzi kupitia Sekretarieti
ya TFF itawasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote ya
maadili ili kujadiliwa na kutolewa uamuzi na kamati hiyo.
Vilevile
kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu ni kipindi cha kukata rufani kwenye
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kwa masuala yasiyo ya maadili. Kwa
watakaokata rufani wanatakiwa kuambatanisha na ada ya rufani kwa Katibu
Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya Septemba 6 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment