Msanii Juma Nature
‘Kiroboto’ akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la kuadhimisha miaka 16 ya kazi
zake za muziki nchini pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za
Kituo cha Redio cha EFM linalofahamika kwa jina la Komaa Concert
litakalofanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi Ukumbi wa Dar Live Mbagala
kuanzia saa 12 jioni. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na
Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo, ambao ni waandaaji
wa tamasha hilo. Kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya
Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha
hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya
Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo
(katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Msanii Said
Christopher ‘Mucky), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya
Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha
hilo,Msanii Juma Nature, Msanii Semani Jabiri ‘Msagasumu’ na Msanii
Snura Mushi.
Wasanii watakaotoa burudani
la nguvu siku hiyo ya tamasha. Kutoka kulia, Fredy Felix ‘Fredwayne’
Juma Nature, Snura Mushia, na Said Christopher ‘Mucky’
Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Lydia Moyo (kushoto), akiperuzi simu yake katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KOMAA CONCERT
Tamasha kubwa la kuadhimisha
miaka kumi na sita ya msanii JUMA NATURE maarufu kama kiroboto pamoja
na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika kama
KOMAA CONCERT kwa mara ya kwanza litafanyika rasmi jumamosi hii ya
tarehe 30 mwezi mei katika ukumbi wa Dar Alive –Mbagala, kuanzia saa
kumi na mbili jioni.
Tamasha hili limeandaliwa na
Juma nature akishirikiana na EFM kwa lengo la kuwaburudisha Mashabiki wa
juma nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru
mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka kumi na sita ya muziki tangu
kuanza msanii huyo Juma Nature aingie kwenye game ya Muziki nchini
Tanzania.
Aidha, mashabiki watapata
burudani kutoka kwa kiroboto ambaye atatumia dakika 180 akiwa jukwaani
kuhakikisha anakonga nyoyo za mashabiki wake ambapo ataimba nyimbo zake
zote kali zilizofanya vizuri na kusindikizwa na wasanii kibao.
Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi.
Tunatoa wito kwa mashabiki wote
wa juma nature , Efm Radio, wadau na wengine kujitokeza kwa wingi siku
ya tamasha hili ili kupata burudani hii ya kihistoria ambapo kiingilio
kitakuwa ni shilingi 7,000 tu.
Tunaamini Juma nature ni msanii
mwenye kipaji kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika
muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa
mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi kipya.
Lakini kwa Efm huyu ni msanii
wa Kwanza itaendelea kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwakuwa kwetu
sisi tunaamini Muziki unaongea.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com)
IMETOLEWA NA, DENIS SSEBO,
MENEJA MAWASILIANO NA MAMBO YA SHERIA WA EFM
No comments:
Post a Comment